JE, MTU AKIMFUATA KRISTO ANAPATA NINI?
Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.
Mathayo 11:28
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Mtu akimfuata Kristo atapata raha nafsini mwake sababu atampumzisha iwapo ana masumbuko na amelemewa na mizigo. Ujitie nira yake na kujifunza kutoka kwake sababu yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo. Na kuanzia hapo mtu anakuwa mwanafunzi wa Kristo, maana yeye amekabidhiwa vyote na Baba, Bwana wa mbingu na nchi, mambo aliyowaficha wenye hekima na akili. Hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia. Nira ya Kristo ni laini, na mzigo wake ni mwepesi.
Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo.
Yeremia 6:16
Kwa maana huku ndiko kumpenda Mungu, kwamba tuzishike amri zake; wala amri zake si nzito.
1 Yohana 5:3
Comments
Post a Comment