JE, MTU AKIWA NDANI YA KRISTO, AMEKUWA NINI?
Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya.
2 Wakorintho 5:17
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. AMEKUWA KIUMBE KIPYA. Hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu, hawafuati mwili bali wafuata roho. Na Kristo akiwa ndani yako, mwili wako umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yako i hai, kwa sababu ya haki. Kristo Yesu asiyejua dhambi alifanywa kuwa dhambi wa ajili yetu, ili tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani.
Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli.
Ufunuo wa Yohana 21:5
Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu.
Wagalatia 6:17
Comments
Post a Comment