JE, MTU AKIZALIWA MARA YA PILI ATAFANYA NINI?
Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye.
1 Yohana 2:29
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Kama mtu akizaliwa mara ya pili atakuwa mtenda haki. Atadumu katika kujitakasa kama Baba alivyo mtakatifu. Mtu na asiwadanganye; atendaye haki yu na haki kama yeye alivyo na haki. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala asiyempenda ndugu yake, maana tumesikia tangu mwanzo, tupendane sisi kwa sisi.
Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye.
1 Yohana 3:1
Comments
Post a Comment