JE, MTU ALIYEZALIWA NA MUNGU ATAIZINGATIA DHAMBI?
Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu.
1 Yohana 3:9
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Atendaye dhambi afanya uasi, kwa sababu dhambi ni uasi. Na atendaye dhambi ni wa ibilisi, na ibilisi alitenda dhambi tangu mwanzo; hivyo Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi zake huyo ibilisi. Lisilo la haki ni dhambi.
Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.
1 Yohana 5:18
Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.
1 Petro 1:23
Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu.
Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu.
Yohana 17:15-16
Comments
Post a Comment