JE, MTU ANAWEZA KUZALIWA NA ROHO, NA BADO AKAFUATA MAMBO YA MWILI?
Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
Yohana 3:6
Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho.
Warumi 8:5
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Hatuna budi kuzaliwa mara ya pili. Aliyezaliwa na roho, hatakiwi kufuata mambo ya mwili. Sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu inatuweka huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Ni ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, hivyo wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu.
Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki.
Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu.
Warumi 8:10,14
Comments
Post a Comment