JE, MTU ANAWEZAJE KUUONA UFALME WA MUNGU?
Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu.
Yohana 3:3
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Usipoongoka na kuwa kama vitoto, hautaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Yoyote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto mdogo, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme huo. Na azishike amri. Mtu lazima azaliwe kwa maji na kwa Roho, ili aingie katika ufalme huo. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho.
Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele.
1 Petro 1:23
Comments
Post a Comment