JE, MUNGU AMEWAWEKEA NINI WATAUWA?
Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa; Bwana atasikia nimwitapo.
Zaburi 4:3
Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi.
Ufunuo wa Yohana 3:10
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Atawasikia wawitapo na kuwaokoa na majaribu. Bwana ajua kuwaokoa wataua na majaribu na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu. Mungu ni mwaminifu na hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo. Na katika jaribu atafanya mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili.
Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.
1 Wakorintho 10:12
Comments
Post a Comment