JE, NI NANI PEKEE ATARUHUSIWA KUMWONA MUNGU?
Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu.
Mathayo 5:8
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili wala hakuapa kwa hila ndicho kizazi cha wautafutao uso wa Mungu. Hakika Mungu ni mwema kwa hao walio safi mioyo yao. Sasa tu wana wa Mungu, haijadhihirika bado tutakavyokuwa ; lakini tunafahamu kuwa tutafanana naye.
Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
Zaburi 51:10
Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu.
1 Yohana 3:3
Comments
Post a Comment