JE, NI NINI KINAIPA DHAMBI NGUVU YA KUUA?
Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati.
1 Wakorintho 15:56
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Je, torati ni dhambi? Hasha! Tusingalitambua dhambi ila kwa sheria, sababu tusingalijua kutamani, kama torati isingalisema, usitamani. Dhambi bila sheria imekufa, na ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yetu kila namna ya kutamani. Tumekwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, tumekuwa watumwa wa haki na kufanywa watumwa wa Mungu.
Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema.
Warumi 7:12
Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake;
Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema.
Warumi 6:12,14
Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Warumi 6:23
Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
1 Wakorintho 15:57
Comments
Post a Comment