JE, NI SAHIHI KUMWITA MTU MCHAFU AU NAJISI?
Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi.
Petro alipokuwa akiingia Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia. Lakini Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwanadamu.
Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu awaye yote mchafu wala najisi.
Matendo ya Mitume 10:15,25-26,28
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Siyo sahihi, na Mungu alionya, asiitwe mtu awaye yote mchafu wala najisi. Hii ilipelekea Petro kutambua ya kuwa Mungu hana upendeleo na katika kila taifa mtu amchaye Mungu na kutenda haki hukubaliwa na yeye.
wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; twawahubiri habari njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;
ambaye zamani zilizopita aliwaacha mataifa yote waende katika njia zao wenyewe.
Matendo ya Mitume 14:15-16
Petro alipokuwa akisema maneno hayo Roho Mtakatifu akawashukia wote waliolisikia lile neno.
Matendo ya Mitume 10:44
Comments
Post a Comment