JE, NI USHINDI GANI AMBAO HATIMAYE WATAPEWA WALE AMBAO WAMEZALIWA MARA YA PILI?
Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu.
1 Yohana 5:4
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Aliyezaliwa na Mungu atapewa kuushinda ulimwengu kwa imani. Mwenye kuushinda ulimwengu ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Na ushindi unapatikana kwa sababu aliye ndani yetu ni mkuu kuliko aliye katika dunia. Tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo.
Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu.
Yohana 16:33
Comments
Post a Comment