Skip to main content

JE, WATU WAKISHAKUWA WANAFUNZI WA KRISTO, WANATAKIWA KUWA NA NIA GANI?

JE, WATU WAKISHAKUWA WANAFUNZI WA KRISTO, WANATAKIWA KUWA NA NIA GANI?

Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu;
Wafilipi 2:5

Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Ikiwako faraja ya Kristo, ushirika wa Roho wa Mungu, hutuma na rehema, ijalizeni furaha ya Kristo ili mwe na nia moja, mapenzi mamoja, roho moja, mkinia mamoja; wala msitende neno lolote kwa majivuno ila kwa unyenyekevu, na kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe bali pia na aangalie mambo ya wengine. Kristo, mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, na akaona kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho; akajifanya hana utukufu, akatwaa namna ya utumwa , akawa mfano wa mwanadamu, akijinyenyekeza na kuwa na utii hata mauti ya msalaba.

Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
Warumi 12:10

Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake.
vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo yote, nisitake faida yangu mwenyewe, ila faida yao walio wengi, wapate kuokolewa.
1 Wakorintho 10:24,33

Comments

Popular posts from this blog

JE, NI MATENDO GANI YALIYO YA MWILI?

JE, NI MATENDO GANI YALIYO YA MWILI? Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Wagalatia 5:19-21 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tuwe makini hapa, matendo ya mwili sio tuu hayo tuliyoambiwa hapo, ila ni pamoja na yanayofanana na hayo. Kuishi katika Kristo ni kuusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Ni kujiepusha na maovu na kujitenga kabisa na matendo mabaya ya mwili. Basi walio katika Kristo waenende kwa Roho, wala hawatatimiza kamwe tamaa za mwili. Mwili hutamani ukishindana na Roho. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufal...

MAWAZO YA MUNGU NA NJIA ZAKE SI MAWAZO YETU WALA NJIA ZETU.

MAWAZO YA MUNGU NA NJIA ZAKE SI MAWAZO YETU WALA NJIA ZETU. Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.     Mawazo yake si mawazo yetu, wala njia zetu si njia zake; kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zake zi juu sana kuliko njia zetu, na mawazo yake kuliko mawazo yetu, asema BWANA. Hivyo tumtafute BWANA, maadamu anapatikana, na tumwite, maadamu yu karibu. Mtu mbaya na uache njia yako, na usiye haki uache mawazo yako, umrudie BWANA naye atakurehemu, urejee kwa Mungu wetu, naye atakusamehe kabisa. Anayajua mawazo anayokuwazia wewe, ni mawazo ya amani, wala si ya mabaya, kukupa wewe tumaini siku zako za mwisho.   Nawe utamwita, utaenda na kumuomba, naye atakusikiliza; utamtafuta, na kumuona, utakapomtafuta kwa moyo wako wote.     BWANA asema hivi, Niite, name nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Na itakuwa kila atakayeliitia jina la B...

TU WARITHI PAMOJA NA KRISTO

TU WARITHI PAMOJA NA KRISTO Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Warumi 8:16-17 Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Wagalatia 4:7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Ufunuo wa Yohana 21:7