Skip to main content

JE, AHADI ZA MUNGU ZIMEWEKWA ULIMWENGUNI KWA SABABU GANI?

JE, AHADI ZA MUNGU ZIMEWEKWA ULIMWENGUNI KWA SABABU GANI?

Tena kwa hayo ametukirimia ahadi kubwa mno, za thamani, ili kwamba kwa hizo mpate kuwa washirika wa tabia ya Uungu, mkiokolewa na uharibifu uliomo duniani kwa sababu ya tamaa.
2 Petro 1:4

Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Ni ili tupate kuwa washarika wa tabia za Uungu, tukiokolewa na uharibifu uliomo humu duniani unaosababishwa na tamaa. Ametukirimia vitu vyote vipasavyo uzima na utauwa kwa kumjua yeye aliyetuita kwa utukufu wake na wema wake mwenyewe. Tujitahidi sana kwa upande wetu, katika imani yetu tutie na wema, katika wema wetu maarifa, katika maarifa yetu kiasi, katika kiasi chetu saburi, katika saburi yetu utauwa, katika utauwa wetu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, UPENDO.

Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
1 Petro 2:9

mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa kama mianga katika ulimwengu,
Wafilipi 2:15

Comments

Popular posts from this blog

JE, NI MATENDO GANI YALIYO YA MWILI?

JE, NI MATENDO GANI YALIYO YA MWILI? Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Wagalatia 5:19-21 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tuwe makini hapa, matendo ya mwili sio tuu hayo tuliyoambiwa hapo, ila ni pamoja na yanayofanana na hayo. Kuishi katika Kristo ni kuusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Ni kujiepusha na maovu na kujitenga kabisa na matendo mabaya ya mwili. Basi walio katika Kristo waenende kwa Roho, wala hawatatimiza kamwe tamaa za mwili. Mwili hutamani ukishindana na Roho. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufal...

TU WARITHI PAMOJA NA KRISTO

TU WARITHI PAMOJA NA KRISTO Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Warumi 8:16-17 Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Wagalatia 4:7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Ufunuo wa Yohana 21:7

MAWAZO YA MUNGU NA NJIA ZAKE SI MAWAZO YETU WALA NJIA ZETU.

MAWAZO YA MUNGU NA NJIA ZAKE SI MAWAZO YETU WALA NJIA ZETU. Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.     Mawazo yake si mawazo yetu, wala njia zetu si njia zake; kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zake zi juu sana kuliko njia zetu, na mawazo yake kuliko mawazo yetu, asema BWANA. Hivyo tumtafute BWANA, maadamu anapatikana, na tumwite, maadamu yu karibu. Mtu mbaya na uache njia yako, na usiye haki uache mawazo yako, umrudie BWANA naye atakurehemu, urejee kwa Mungu wetu, naye atakusamehe kabisa. Anayajua mawazo anayokuwazia wewe, ni mawazo ya amani, wala si ya mabaya, kukupa wewe tumaini siku zako za mwisho.   Nawe utamwita, utaenda na kumuomba, naye atakusikiliza; utamtafuta, na kumuona, utakapomtafuta kwa moyo wako wote.     BWANA asema hivi, Niite, name nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Na itakuwa kila atakayeliitia jina la B...