JE, AMRI YA KIFO ILITEKELEZWAJE KWA ADAMU?
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Mungu akasema, kwa sababu huyu mtu amejua mema na mabaya, na amekuwa kama mmoja wetu, asije tena akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala akaishi milele; akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi upande wa masharikiwa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima. Akamtoa katika bustani ya Edeni, ailime ardhi ambayo katika hiyo alitwaliwa.
Hivyo, mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu. Basi kwa jinsi hiyo Mungu aliupenda ULIMWENGU kiasi cha kumtoa mwana wake pekee, mpendwa, ili KILA AMWAMINIYE asipotee, bali awe na uzima wa milele. Mungu amemtuma Mwanawe ili tupate uzima wa yeye, na kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu. Si kwamba sisi tulimpenda, bali yeye alitupenda sisi.
Mwanzo 3:22,24,23, Warumi 6:23,
Yohana 3:16 & 1 Yohana 4:9-10.
Comments
Post a Comment