JE, INJILI ILIHUBIRIWA ZAMANI, KAMA WAKATI WA IBRAHIMU?
Na andiko, kwa vile lilivyoona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani, lilimhubiri Ibrahimu habari njema zamani, kusema, Katika wewe Mataifa yote watabarikiwa.
Wagalatia 3:8
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Kama Ibrahimu alivyomwamini Mungu wa mbinguni akahesabiwa haki, hivyo tufahamu kuwa wale walio wa imani, hao ndio wana wa Ibrahimu, nao hubarikiwa pamoja na Ibrahimu aliyekuwa na imani. Andiko lilimhubiria Ibrahimu habari njema zamani, kwamba katika yeye Mataifa yote watabarikiwa, sababu liliona tangu zamani kwamba Mungu atawahesabia haki Mataifa kwa imani. Na katika yeye mataifa yote ya dunia watabarikiwa.
nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa.
Mwanzo 12:3
Naam, na manabii wote tangu Samweli na wale waliokuja baada yake, wote walionena, walihubiri habari za siku hizi. Ninyi mmekuwa watoto wa manabii na wa maagano yale, ambayo Mungu aliagana na baba zenu, akimwambia Ibrahimu, Katika uzao wako kabila zote za ulimwengu zitabarikiwa.
Matendo ya Mitume 3:24-25
Comments
Post a Comment