JE, KANISA LA KIKRISTO LIMEJENGWA JUU YA MSINGI GANI?
Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni.
Waefeso 2:20
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Bwana, MUNGU, asema hivi, Tazama, naweka jiwe katika Sayuni, liwe msingi, jiwe lililojaribiwa, jiwe la pembeni lenye thamani, msingi ulio imara. Katika Kristo jengo lote linaunganishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana, na katika yeye tunajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.
Simoni Petro akajibu akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala milango ya kuzimu haitalishinda.
Mathayo 16:16,18
Comments
Post a Comment