JE, MTU ANAWEZA KUOKOLEWA BILA IMANI?
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye tumepata kwa njia ya imani kuifikia neema ambayo tunasimama ndani yake, na kufurahi katika tumaini la utukufu wa Mungu. Tunahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu, ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani ya damu yake. Hivyo mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria.
Mwenye haki wa Mungu ataishi kwa imani, ila akisitasita roho yake haitakuwa na furaha naye. Sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwa walio na imani ya kutuokoa roho zetu. Na ni dhahiri kuwa, hakuna mtu ahesabiwaye haki mbele za Mungu katika sheria. Pasipo imani haiwezekani kumpendeza Mungu, maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na huwapa thawabu wale wamtafutao. Tusiutupe ujasiri wetu maana una thawabu kuu.
Warumi 5:1-2, Warumi 3:24-25,28,
Waebrania 10:38-39, Wagalatia 3:11, Waebrania 11:6, Waebrania 10:35.
Comments
Post a Comment