JE, MUNGU AMEWEKA MIPANGO MINGAPI YA WOKOVU?
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hapana jina jingine chini ya mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.
Matendo ya Mitume 4:12
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Ameweka mpango mmoja tuu, nao ni wanadamu kuokolewa kwa jina moja, nalo ni jina la Kristo Yesu. Yusufu, mwana wa Daudi aliambiwa na malaika katika ndoto kuwa, asihofu na amchukue Mariamu mkewe, maana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu; atazaa mwana na wamwite jina lake Yesu, maana ndiye atakayewaokoa watu wake na dhambi zao.
Comments
Post a Comment