JE, MUSA ALIMWAMINI KRISTO?
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Kwa imani Musa alipozaliwa, alifichwa miezi mitatu na wazazi wake bila kuogopa amri ya mfalme; na kwa imani alipokuwa mtu mzima alikataa kuitwa mwana wa binti Farao, akiona ni afadhali kupata mateso pamoja na watu wa Mungu kuliko kujifurahisha katika dhambi kwa muda; akihesabu ya kuwa kushutumiwa kwake Kristo ni utajiri mkuu kuliko hazina za Misri, kwa kuwa aliyatazamia hayo malipo. Kwa imani hakuogopa ghadhabu ya mfalme, akatoka Misri, maana alistahimili kama amwonaye yeye asiyeonekana.
Tusiutupe ujasiri wetu maana una thawabu kuu, tukiwaonea huruma wale walio katika vifungo, na tukikubali kwa furaha kunyang'anywa mali zetu, tukijua nafsini mwetu mna mali iliyo njema zaidi, idumuyo. Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao; tukimtazama Yesu, mwenye kuanzisha na mwenye kutimiza imani yetu, ambaye kwa ajili ya furaha iliyowekwa mbele yake aliustahimili msalaba na kuidharau aibu, naye ameketi mkono wa kuume wa kiti cha enzi cha Mungu.
Waebrania 11:23-27, Waebrania 10:34-35,
Waebrania 13:14, Waebrania 12:2.
Comments
Post a Comment