JE, NI HESHIMA KIASI GANI INAYOSTAHILI KWA KRISTO?
ili watu wote wamheshimu Mwana kama vile wanavyomheshimu Baba. Asiyemheshimu Mwana hamheshimu Baba aliyempeleka.
Yohana 5:23
Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Tunavyomheshimu Baba yetu aliye mbinguni ndivyo tanatakiwa kumheshimu Mwana, yaani Kristo Yesu. Kristo Yesu hakutenda neno mwenyewe ila lile ambalo Baba analitenda, tena amempa yeye hukumu yote. Tena Mungu alimwadhimisha mno, akamkirimia Jina lile lipitalo kila jina, ili kwa jina la Yesu kila goti lipigwe na kila ulimi ukiri ya kuwa YESU KRISTO NI BWANA, kwa utukufu wa Mungu Baba. Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; na amkiriye Mwana anaye Baba pia.
Awasikilizaye ninyi anisikiliza mimi, naye awakataaye ninyi anikataa mimi; naye anikataaye mimi amkataa yeye aliyenituma.
Luka 10:16
Comments
Post a Comment