JE, NI NANI ALIYELETA KIFO KWA WANADAMU?
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi. Adamu alionywa matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya asile, kwa maana siku atakapokula matunda ya mti huo atakufa hakika. Baada ya Adamu kutotii maagizo aliyopewa, aliambiwa atairudia ardhi, ambayo katika hiyo alitwaliwa; kwa maana yu mavumbi, na mavumbini atarudi.
Mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. Lakini ashukuriwe Mungu atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo.
Warumi 5:12, Mwanzo 2:17,
Mwanzo 3:19, Warumi 6:23,
1 Wakorintho 15:56-57
Comments
Post a Comment