JE, NI NANI ANAPATA UZIMA WA MILELE?
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Yeye aliye naye Mwana wa Mungu, anao huo uzima; asiye naye Mwana wa Mungu hana huo uzima. Ushuhuda wa Mungu ni kwamba amemshuhudia Mwanawe. Yeye amwaminiye Mwana wa Mungu anao huo ushuhuda ndani yake asiyeamini huo ushuhuda, amemfanya Mungu kuwa mwongo. Na huo ushuhuda ni kwamba Mungu alitupa uzima wa milele, na uzima huu umo katika Mwanawe.
Amwaminiye Mwana wa Mungu yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia. Amwaminiye hahukumiwi, bali asiyemwamini amekwisha kuhukumiwa kwa kutoliamini jina la Mwana pekee wa Mungu. Roho wa Mungu anashuhudia na roho zetu kuwa sisi tu watoto wa Mungu.
Mungu aliupenda ulimwengu na akamtoa mwanawe pekee ili kila mtu amwaminiye awe na uzima wa milele.
1 Yohana 5:9-12, Yohana 3:36,18,
Warumi 8:16, Yohana 3:16.
Comments
Post a Comment