Skip to main content

JE, WAMWAMINIJE YEYE WASIYEMSIKIA?

JE, WAMWAMINIJE YEYE WASIYEMSIKIA?

    Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.
    Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema!
    Lakini si wote walioitii ile habari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu? Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako, na ni lile neno la imani tulihubirilo.
    Hivyo basi, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na ukaamini moyoni mwako ya kuwa Mungu Baba yetu wa Mbinguni alimfufua katika wafu utaokoka. Maana kwa moyo mtu huamini na kupata haki, na kwa kinywa mtu hukiri na kupata wokovu.
    Sasa basi kumwamini Kristo Yesu usiyemsikia huja kwa kusoma neno la Kristo ambalo ni neno la Mungu Baba yetu, na kutoka kwa wahubirio habari ya mema. Kwa maana hatujihubiri wenyewe, bali Kristo Yesu ya kuwa ni Bwana  na sisi wenyewe kuwa tu watumishi wenu kwa ajili ya Yesu. Kwa kuwa maneno aliyopewa Kristo Yesu alitupa kupitia wanafunzi wake, nao wakayapokea na wakajua hakika kuwa ametoka kwa Baba yetu mbinguni na kusadiki kwamba yeye ndiye aliyemtuma.

Warumi 10, 2 Wakorintho 4:5,
Yohana 17:8

Comments

Popular posts from this blog

JE, NI MATENDO GANI YALIYO YA MWILI?

JE, NI MATENDO GANI YALIYO YA MWILI? Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Wagalatia 5:19-21 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tuwe makini hapa, matendo ya mwili sio tuu hayo tuliyoambiwa hapo, ila ni pamoja na yanayofanana na hayo. Kuishi katika Kristo ni kuusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Ni kujiepusha na maovu na kujitenga kabisa na matendo mabaya ya mwili. Basi walio katika Kristo waenende kwa Roho, wala hawatatimiza kamwe tamaa za mwili. Mwili hutamani ukishindana na Roho. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufal...

TU WARITHI PAMOJA NA KRISTO

TU WARITHI PAMOJA NA KRISTO Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Warumi 8:16-17 Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Wagalatia 4:7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Ufunuo wa Yohana 21:7

MAWAZO YA MUNGU NA NJIA ZAKE SI MAWAZO YETU WALA NJIA ZETU.

MAWAZO YA MUNGU NA NJIA ZAKE SI MAWAZO YETU WALA NJIA ZETU. Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.     Mawazo yake si mawazo yetu, wala njia zetu si njia zake; kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zake zi juu sana kuliko njia zetu, na mawazo yake kuliko mawazo yetu, asema BWANA. Hivyo tumtafute BWANA, maadamu anapatikana, na tumwite, maadamu yu karibu. Mtu mbaya na uache njia yako, na usiye haki uache mawazo yako, umrudie BWANA naye atakurehemu, urejee kwa Mungu wetu, naye atakusamehe kabisa. Anayajua mawazo anayokuwazia wewe, ni mawazo ya amani, wala si ya mabaya, kukupa wewe tumaini siku zako za mwisho.   Nawe utamwita, utaenda na kumuomba, naye atakusikiliza; utamtafuta, na kumuona, utakapomtafuta kwa moyo wako wote.     BWANA asema hivi, Niite, name nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Na itakuwa kila atakayeliitia jina la B...