MPINGA KRISTO YUAJA, NA WENGI WAMEKUWEPO.
Neema na amani na ziongezwe kwetu.
Ni wakati wa mwisho, na kama mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja; sio hivyo tuu hata wakati huo walikuwepo. Tumepakwa mafuta na yeye akiye mtakatifu, hivyo tunajua yote. Hatukuandikiwa sisi kwa sababu hatujui iliyo kweli, bali kwa sababu tunaijua, tena hakuna uongo wo wote utokao katika hiyo kweli. Aliye mwongo ni yule akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo; na huyu ndiye mpinga Kristo, amkanaye Baba na Mwana. Basi tulilosikia tangu mwanzo likikaa ndani yetu nasi tutakaa ndani ya Mwana, na ndani ya Baba.
Kila roho isiyomkiri Yesu haitokani na Mungu, na hii ndio roho ya mpinga Kristo ambayo tumesikia yaja, na sasa tayari imekwisha kuwako duniani. Hivyo tusiamini kila roho, bali tuzijaribu hizo roho kama zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. Twamjua Roho wa Mungu, na kila roho ikiriyo kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatokana na Mungu.
Tujihadhari na manabii wa uongo, watu waliovalia mavazi ya kondoo kumbe ndani ni mbwa-mwiti wakali. Tusimzimishe Roho wala tusitweze unabii, bali tujaribu mambo yote kwa kulishika lililo jema na kwa kujitenga na ubaya wa kila. Ukimjua Mungu, utumjua Roho wa kweli na roho ya upotevu.
1 Yohana 2:18-22,24, 1 Yohana 4:3,1,2,
Mathayo 7:15
Comments
Post a Comment