MTAFUTE BWANA KWA MOYO WAKO WOTE.
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Utamtafuta na kumuona, utakapomtafuta kwa moyo wako wote. Maana anajua mawazo anayokuwazia wewe, asema BWANA, ni mawazo ya amani, wala si mabaya, kukupa wewe tumaini siku zako za mwisho. Utamwita, utakwenda na kumuomba, naye atakusikiliza na ataonekana kwako. Naye atakupa moyo, umjue ya kuwa yeye ni BWANA; nawe utakuwa mtu wake, naye atakuwa Mungu wako; kwa maana utamrudia kwa moyo wako wote.
Ombeni nanyi, mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa. Mwaminini Mungu, na yo yote myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu. Na mkiomba lo lote kwa jina la Kristo Yesu, hilo atalifanya yeye Kristo, ili Baba atukuzwe ndani ya Mwana.
Yeremia 29:11-13, Yeremia 24:7, Mathayo 7:7, Marko 11:22, Yohana 14:13.
Comments
Post a Comment