MTAKUWA WATAKATIFU KWA KUWA YEYE NI MTAKATIFU.
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Heri wenye kuudhiwa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao. Tujapoteswa kwa sababu ya haki tuna heri. Tusiogope kutisha kwao wala tusifadhaike , bali tumtakase Kristo Bwana mioyoni mwetu. Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki, na masikio yake husikiliza maombi yao. Hakuna wa kutudhuru, tukiwa wenye juhudi katika mema. Tukistahimili tutendapo matendo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.
Tumjibu kila mtu habari za tumaini lililo ndani yetu, kwa upole na kwa hofu. Tuwe na dhamiri njema, ili lile neno tunalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wetu mwema katika Kristo. Tuwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili kwa kutusingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yetu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
Mungu Baba yetu, kwa rehema zake nyingi alituzaa mara ya pili ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwake Yesu Kristo katika wafu. Tuwe na kiasi, tukiitumainia kwa utimilifu ile neema katika ufunuo wa Yesu Kristo; kama watoto wa kutii tusijifananishe na taama za kwanza za ujinga wetu, bali kama yeye alivyo mtakatifu, nasi tuwe watakatifu katika mienendo yetu yote; kwa maana imeandikwa, tutakuwa watakatifu kwa kuwa yeye ni mtakatifu.
Mathayo 5:10, 1 Petro 3:12-16,
1 Petro 2:20,12, 1 Petro 1:3,13-16.
Comments
Post a Comment