NENO LA UJUMBE LA MUNGU.
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu.
Mnapopata neno la ujumbe la Mungu, mnalolisikia kwa watumishi wa Mungu au kwa kusoma maandiko, mlipokee si kama neno la mwanadamu, bali kama neno la Mungu; na ndivyo lilivyo kweli kweli, na litendavyo kazi ndani yenu ninyi mnaoamini. Injili aliyoihuiri Mtume Paulo, aliwajulisha sio ya namna ya kibinadamu, kwa kuwa hakupokea kwa mwanadamu wala hakufundishwa na mwanadamu, bali kwa ufunuo wa Yesu Kristo. Mungu ametuchagua tangu mwanzo tupate wokovu, katika kutakaswa na Roho, na kuiamini kweli aliyotuitia kwa injili, ili kuupata utukufu wa Bwana wetu Yesu Kristo. Basi ndugu, msimame imara kwa kuyashika mapokeo ya kweli mnayofundishwa, ama kwa maneno, ama kwa waraka wa mitume. Basi mlipokee lile neno kwa uelekevu wa moyo, mkiyachunguza maandiko kila siku, muone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.
1 Wathesalonike 2: 13, Wagalatia 1:11,
2 Wathesalonike 2:13, Matendo ya Mitume 17: 11
Comments
Post a Comment