TUWE WATENDAJI WA NENO.
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Imani chanzo chake ni kusikia, na kusikia huja kwa neno la Kristo. Imani hukua kwa kusikia neno la Kristo kila wakati, usiku na mchana, bila kuchoka, na kulitenda neno. Hivyo basi, tuweke mbali uchafu wa kila namna, na kupokea lile neno lipandwalo ndani yetu ili kuokoa roho zetu; na tuwe watendaji wa neno, wala si wasikiaji tuu, huku tukidanganya nafsi zetu. Na imani bila matendo imekufa.
Maana ukiwa ni msikiaji wa neno na si mtendaji, unafanana na mtu yule anayejiangalia uso wake kwenye kioo; hujiangalia kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo. Hivyo, yeye ajuaye kutenda mema, na hayatendi, kwake huyo ni dhambi. Asikiaye hayo maneno ya Kristo asiyafanye, atafananishwa na mtu mpumbavu alijejenga nyumba yake juu ya mchanga; mvua ikinyesha, na nyumba hiyo ikapigwa na mafuriko na upepo mkali ikaanguka, tena anguko lake likawa kubwa. Hivyo basi, sio kila mtu asemaye Bwana, Bwana atakayeingia katika ufalme wa mbinguni, bali ni wale wafanyao mapenzi ya Mungu, Baba yetu aliye mbinguni.
Warumi 10:17, Yakobo 1:21-24,
Yakobo 2:26, Yakobo 4:17,
Mathayo 7:26-27,21.
Comments
Post a Comment