Skip to main content

UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA.

  UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA.

NEEMA NA IWE KWENU, NA AMANI, ZITOKAZO KWA MUNGU BABA YETU KATIKA KRISTO YESU.
    WAKATI UMETIMIA, NA UFALME WA MUNGU UMEKARIBIA; TUBUNI NA KUIAMINI INJILI. UFALME WA MUNGU NI HAKI NA AMANI NA FURAHA KATIKA ROHO MTAKATIFU. UTAFUTENI KWANZA UFALME WA MUNGU NA HAKI YA MUNGU. TORATI NA MANABII VILIKUWAPO MPAKA YOHANA, NA TOKEA WAKATI HUO HABARI NJEMA YA UFALME WA MUNGU HUTANGAZWA, NA KILA MTU HUJIINGIZA KWA NGUVU.
    TANGU SIKU ZA YOHANA MBATIZAJI HATA SASA UFALME WA MBINGUNI HUPATIKANA KWA NGUVU, NAO WENYE NGUVU WAUTEKA, MAANA MANABII WOTE NA TORATI WALITABIRI MPAKA WAKATI WA YOHANA, NA YEYE NDIYE ELIYA ATAKAYEKUJA. MWENYE MASIKIO NA ASIKIE. JITAHIDINI KUINGIA KATIKA MLANGO ULIO MWEMBAMBA, KWA MAANA WENGI WATATAKA KUINGIA WASIWEZE.
    KWA MAANA HATUKUJA NA KITU DUNIANI, HIVYO HATUWEZI KUTOKA NA KITU. SHINA MOJA LA MABAYA YA KILA NAMNA NI KUPENDA FEDHA, AMBAPO WENGI WAMEFARAKANA NA IMANI KWA KUPENDA HILO. BALI WEWE MTU WA MUNGU UYAKIMBIE MAMBO HAYO, UKAFUATE HAKI, UTAUWA, IMANI, UPENDO, SABURI NA UPOLE. PIGA VITA VILE VIZURI VYA IMANI, UKISHIKA UZIMA ULE WA MILELE ULIOITIWA, UKIUNGAMA MAUNGAMO MAZURI MBELE YA MASHAHIDI WENGI, KWAMBA UILINDE AMRI HII PASIPO MAWAA, PASIPO LAWAMA, HATA KUFUNULIWA KWAKE BWANA WETU YESU KRISTO, YEYE ALIYEHIMIDIWA, MWENYE UWEZA PEKE YAKE, MFALME WA WAFALME, BWANA WA MABWANA.
   

Marko 1:15, Warumi 14:17, Mathayo 6:33,
Luka 16:16, Mathayo 11:12-15,
Luka 13:24, 1 Timotheo 6:7,10-15

Comments

Popular posts from this blog

JE, NI MATENDO GANI YALIYO YA MWILI?

JE, NI MATENDO GANI YALIYO YA MWILI? Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Wagalatia 5:19-21 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu. Tuwe makini hapa, matendo ya mwili sio tuu hayo tuliyoambiwa hapo, ila ni pamoja na yanayofanana na hayo. Kuishi katika Kristo ni kuusulubisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Ni kujiepusha na maovu na kujitenga kabisa na matendo mabaya ya mwili. Basi walio katika Kristo waenende kwa Roho, wala hawatatimiza kamwe tamaa za mwili. Mwili hutamani ukishindana na Roho. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufal...

TU WARITHI PAMOJA NA KRISTO

TU WARITHI PAMOJA NA KRISTO Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Warumi 8:16-17 Kama ni hivyo, wewe si mtumwa tena bali u mwana; na kama u mwana, basi, u mrithi kwa Mungu. Wagalatia 4:7 Yeye ashindaye atayarithi haya, nami nitakuwa Mungu wake, naye atakuwa mwanangu. Ufunuo wa Yohana 21:7

MAWAZO YA MUNGU NA NJIA ZAKE SI MAWAZO YETU WALA NJIA ZETU.

MAWAZO YA MUNGU NA NJIA ZAKE SI MAWAZO YETU WALA NJIA ZETU. Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.     Mawazo yake si mawazo yetu, wala njia zetu si njia zake; kwa maana kama vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zake zi juu sana kuliko njia zetu, na mawazo yake kuliko mawazo yetu, asema BWANA. Hivyo tumtafute BWANA, maadamu anapatikana, na tumwite, maadamu yu karibu. Mtu mbaya na uache njia yako, na usiye haki uache mawazo yako, umrudie BWANA naye atakurehemu, urejee kwa Mungu wetu, naye atakusamehe kabisa. Anayajua mawazo anayokuwazia wewe, ni mawazo ya amani, wala si ya mabaya, kukupa wewe tumaini siku zako za mwisho.   Nawe utamwita, utaenda na kumuomba, naye atakusikiliza; utamtafuta, na kumuona, utakapomtafuta kwa moyo wako wote.     BWANA asema hivi, Niite, name nitakuitikia, nami nitakuonyesha mambo makubwa, magumu usiyoyajua. Na itakuwa kila atakayeliitia jina la B...