UPENDO WA MUNGU KWETU.
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Mungu, Baba yetu aliye mbinguni, alionyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Maana hapo tulipokuwa hatuna nguvu, wakati ulipotimia, Kristo alikufa kwa ajili ya waovu. Tulipokuwa adui, tulipatanishwa na Mungu kwa mauti ya Mwana wake; zaidi sana baada ya kupatanishwa tutaokolewa katika uzima wake na twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumepokea huo upatanisho.
Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele; na hakumtuma Mwana ulimwenguni kuhukumu ulimwengu, bali ulimwengu uokolewe katika yeye. Hili ndilo pendo, si kwamba sisi tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda sisi, akamtuma Mwanawe kuwa kipatanisho kwa dhambi zetu.
Wapenzi, na tupendane, sababu pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu na anamjua Mungu , kwa maana Mungu ni upendo. Ikiwa Mungu ametupenda sisi hivi, imetupasa na sisi kupendana. Hakuna mtu aliyemwona Mungu wakati wo wote. Tukipendana, Mungu hukaa ndani yetu na sisi tunakaa ndani yake, na pendo lake linakamilika ndani yetu, kwa kuwa ametushirikisha Roho wake.
Warumi 5:6-11, Yohana 3:16,
1 Yohana 4:7-13.
Comments
Post a Comment