Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2020

WAPANDAO WALA WATIAO MAJI SI KITU, BALI AKUZAYE.

WAPANDAO WALA WATIAO MAJI SI KITU, BALI AKUZAYE. Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.     Apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. Hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu?   Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? Basi Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.     Yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.     Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa ...

NI NINI MATOKEO YA KUANGUKA KWA MWANADAMU?

NI NINI MATOKEO YA KUANGUKA KWA MWANADAMU? Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.     Kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi. Bali Mungu aonyesha pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu, tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki na kutii kwake mmoja watu wote wameingizwa katika hali ya wenye haki na walihesabiwa haki yenye uzima. Na wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa yule mmoja, Yesu Kristo. Tumekwisha kuhesabiwa haki katika damu yake, tumeokolewa na ghadhabu kwa yeye. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo upatanisho.     Mungu alimwagiza huyo mtu aliyeingiza dhambi,...

JE, NI KWA NAMNA GANI BIBLIA INAELEZA HABARI ZA WALIOLALA MAUTI?

JE, NI KWA NAMNA GANI BIBLIA INAELEZA HABARI ZA WALIOLALA MAUTI? Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.     Tunatakiwa tujue habari zao waliolala mauti ili tusihuzunike kama na wengine waliokosa matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye; na watakaokuwa hai hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo ( WALIOLALA KATIKA YESU ) watafufuliwa kwanza, kisha walio hai, waliosalia, watanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili wamlaki Bwana hewani; na hivyo watakuwa pamoja na Bwana milele.     Maana, kama wafu hawafufuliwi , Kristo naye hakufufuka, na kama hakufufuka, imani yetu ni bure, tungalimo katika dhambi zetu. Lakini sasa Kri...