NI NINI MATOKEO YA KUANGUKA KWA
MWANADAMU?
Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na
kwa Bwana Yesu Kristo.
Kwa mtu mmoja
dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti
ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi. Bali Mungu aonyesha
pendo lake yeye mwenyewe kwetu sisi, kwa kuwa Kristo alikufa kwa ajili yetu,
tulipokuwa tungali wenye dhambi. Basi tena, kama kwa kosa moja watu wote
walihukumiwa adhabu, kadhalika kwa tendo moja la haki na kutii kwake mmoja watu
wote wameingizwa katika hali ya wenye haki na walihesabiwa haki yenye uzima. Na
wapokeao wingi wa neema, na kile kipawa cha haki, watatawala katika uzima kwa
yule mmoja, Yesu Kristo. Tumekwisha kuhesabiwa haki katika damu yake,
tumeokolewa na ghadhabu kwa yeye. Wala si hivyo tu, ila pia twajifurahisha
katika Mungu kwa Bwana wetu Yesu Kristo, ambaye kwa yeye sasa tumeupokea huo
upatanisho.
Mungu alimwagiza
huyo mtu aliyeingiza dhambi, akisema, matunda ya kila mti wa bustani waweza
kula, ila ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, maana siku utakapokula
utakufa hakika. Baada ya kutokutii na kula, Mungu akamwambia Adamu ya kwamba
atairudia ardhi ambayo kwa hiyo alitwaliwa, kwa maana yu mavumbi, naye
mavumbini atarudi.
Hivyo, kwa maana
dhambi ililetwa na mtu, kadhalika na kiyama ya wafu ililetwa na mtu. Katika
Adamu wote tunakufa, kadhalika na katika Kristo wote tutahuishwa, kila mmoja
mahali pake; Kristo amefufuka katika wafu, limbuko lao waliolala; baadaye walio
wake Kristo atakapokuja. Mtu wa kwanza, Adamu, nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho
ni roho yenye kuhuisha. Hupandwa mwili wa asili, hufufuliwa mwili wa roho;
ikiwa uko mwili wa asili, na wa roho pia uko.
Warumi 5:8- 19, Mwanzo 2:16-17, Mwanzo 3:17-19,
1 Wakorintho 15:20-23,44,45.
Comments
Post a Comment