WAPANDAO WALA WATIAO
MAJI SI KITU, BALI AKUZAYE.
Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na
kwa Bwana Yesu Kristo.
Apandaye si kitu,
wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye. Hata sasa ninyi ni watu wa tabia ya
mwilini. Maana, ikiwa kwenu kuna husuda na fitina, je! Si watu wa tabia ya
mwilini ninyi; tena mnaenenda kwa jinsi ya kibinadamu? Maana hapo mtu mmoja asemapo, Mimi ni wa
Paulo; na mwingine, Mimi ni wa Apolo, je! Ninyi si wanadamu? Basi Apolo ni
nani? Na Paulo ni nani? Ni wahudumu ambao kwao mliamini; na kila mtu kama Bwana
alivyompa. Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.
Yeye apandaye, na
yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe
sawasawa na taabu yake mwenyewe. Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye
kuuweka, isipokuwa ni ule uliokwisha kuwekwa, yaani, Yesu Kristo.
Hamjui ya kuwa
ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? Mtu
asijidanganye mwenyewe; kama mtu akijiona kuwa mwenye hekima miongoni mwenu
katika dunia hii, na awe mpumbavu, ili apate kuwa mwenye hekima. Maana hekima
ya dunia hii ni upuzi mbele za Mungu, anayafahamu mawazo ya wenye hekima ya
kwamba ni ya ubatili. Basi, mtu ye yote na asijisifie wanadamu, kwamba ni Paulo,
au Apolo, au Kefa; au dunia, au uzima, au mauti; au vile vilivyopo sasa, au
vile vitakavyokuwapo; vyote ni vyenu; nanyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa
Mungu.
Basi ndugu,
nawasihi, kwa jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba nyote mnene mamoja; wala
pasiwe kwenu faraka, bali mhitimu katika nia moja na shauri moja.
1 Wakorintho 3:7,3-6,8,11,16,18-23, 1 Wakorintho 1:10-14.
Comments
Post a Comment