JE, NI KWA NAMNA GANI
BIBLIA INAELEZA HABARI ZA WALIOLALA MAUTI?
Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na
kwa Bwana Yesu Kristo.
Tunatakiwa tujue
habari zao waliolala mauti ili tusihuzunike kama na wengine waliokosa
matumaini. Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo
na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye; na watakaokuwa hai
hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala
mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na
sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo (WALIOLALA KATIKA YESU) watafufuliwa
kwanza, kisha walio hai, waliosalia, watanyakuliwa pamoja nao katika mawingu,
ili wamlaki Bwana hewani; na hivyo watakuwa pamoja na Bwana milele.
Maana, kama wafu
hawafufuliwi , Kristo naye hakufufuka, na kama hakufufuka, imani yetu ni bure,
tungalimo katika dhambi zetu. Lakini sasa Kristo amefufuka katika wafu, limbuko
lao waliolala.
1 Wathesalonike 4:13-17, 2 Wakorintho 15:16-20.
Comments
Post a Comment