HABARI ZAO WALIOLALA MAUTI.
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini.
Maana, ikiwa twaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. Kwa kuwa twawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele.
Basi, farijianeni kwa maneno hayo.
Maswali ni, je, sisi tuliobaki na wale watakaobaki hata wakati wa kuja kwake Bwana tunayo matumaini? Na, je tunakiri kwa vinywa vyetu ya kwamba Yesu ni Bwana na tunaamini kwamba Yesu alikufa na kufufuka kama hao waliolala katika Kristo walivyoamini? Je, tumebaki katika Kristo ili nasi tunyakuliwe pamoja na waliolala katika Kristo kumlaki Bwana hewani na kuwa naye milele?
Hivyo waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza, kisha walio hai katika Kristo watanyakuliwa pamoja nao katika mawingu kumlaki Bwana hewani tuwe pamoja naye milele.
1 Wathesalonike 4:13-18
Comments
Post a Comment