HATUJAPEWA ROHO YA WOGA.
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Tuzichochee karama za Mungu zilizo ndani yetu, maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu, na ya upendo na ya moyo wa kiasi. Hivyo tusiuonee haya ushuhuda wa Bwana wetu, bali tuvumilie mabaya kwa ajili ya Injili, kwa kadiri ya nguvu ya Mungu. Mungu alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa matendo yetu sisi bali kwa makusudi yake yeye na neema yake tuliyopewa katika Kristo Yesu tangu milele.
Tunaoongozwa na Roho wa Mungu, ndio wana wa Mungu na hatukupokea tena roho ya utumwa iletayo hofu, bali tulipokea roho ya kufanywa wana. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu kuwa sisi tu watoto wa Mungu, na tu warithi wa Mungu turithio pamoja na Kristo, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Tumepewa msaidizi, Roho Mtakatifu, ambaye Baba ametupa kwa jina la Kristo Yesu, atufundishe yote, atukumbushe yote ambayo Kristo alituambia. Ndipo Kristo Yesu akatuambia; Amani ametuachia, amani yake ametupa, na alivyotupa yeye sivyo kama ulimwengu utoavyo. Hivyo tusifadhaike mioyoni mwetu, wala tusiwe na woga.
1 Timotheo 1:6-10, Warumi 8:14-17,
Yohana 14:26-27.
Comments
Post a Comment