JE, ILIAMULIWA TANGU MWANZO KWAMBA KRISTO LAZIMA AFE?
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Alionewa, lakini alinyenyekea, Wala hakufunua kinywa chake; Kama mwana-kondoo apelekwaye machinjoni, Na kama vile kondoo anyamazavyo Mbele yao wakatao manyoya yake; Naam, hakufunua kinywa chake. Wakamfanyia kaburi pamoja na wabaya; Na pamoja na matajiri katika kufa kwake; Ingawa hakutenda jeuri, Wala hapakuwa na hila kinywani mwake.
Tunafahamu kwamba tulikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani ya Kristo. Amejulikana tangu zamani kabla haijawekwa misingi ya dunia, lakini alifunuliwa kwa ajili yetu. Mungu alituchagua katika Kristo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
Ufunuo wa Yohana 13:8, Isaya 53:5,7,9,
1 Petro 1:18-20, Waefeso 1:4.
Comments
Post a Comment