KUMPENDA MUNGU NI PAMOJA NA KUZISHIKA AMRI ZAKE.
Neema na amani na ziongezwe kwetu.
Aliye na amri za Kristo, na kuzishika, ndiye ampendaye; naye ampendaye atapendwa na Baba yake, naye Kristo atampenda na kujidhihirisha kwake. Kristo Yesu alisema, Mtu akimpenda, atalishika neno lake, na Baba yaklle atampenda, nao watakuja kwake, na kufanya makao kwake. Na atatambua Kristo yu ndani ya Baba yake, nawe ndani yake, naye Kristo Yesu ndani ya mtu huyo. Roho Mtakatifu ndiye atakayetufundisha yote, na kutukumbusha yote Kristo aliyotuambia.
Tumpendapo Mungu na tuzishike amri zake. Kwa maana huku ndipo kumpenda Mungu, tuzishike amri, na amri zake si nzito. Kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu kwa hiyo imani yetu. Mwenye kuushinda ulimwengu ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Tujitie nira ya Kristo, tujifunze kwake, sababu yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo, nasi tutapata raha nafsini mwetu, maana nira yake ni laini, na mzigo wake ni mwepesi.
Yohana 14:21, 1 Yohana 5:3,
Mathayo 16:33.
Comments
Post a Comment