MTASIKIA WALA HAMTAELEWA, MTATAZAMA WALA HAMTAONA.
NEEMA NA IWE KWENU, NA AMANI, ZITOKAZO KWA MUNGU BABA YETU KATIKA KRISTO YESU.
MMEJALIWA KUZIJUA SIRI ZA UFALME WA MBINGUNI, BALI WAO HAWAKUJALIWA. WAKITAZAMA HAWAONI, NA WAKISIKIA HAWASIKII, WALA KUELEWA. MWENYE KITU ATAPEWA, NAYE ATAZIDISHIWA TELE, LAKINI YE YOTE ASIYE NA KITU, HATA KILE KIDOGO ALICHO NACHO ATANYANG'ANYWA. HERI MACHO YENU, KWA KUWA YANAONA; NA MASIKIO YENU, KWA KUWA YANASIKIA.
MAANA MTU ALISIKIAPO NENO LA UFALME ASIELEWE NALO, HUJA YULE MWOVU AKALINYAKUA LILILOPANDWA MOYONI MWAKE. MWINGINE ALISIKIAYE NENO, AKALIPOKEA MARA KWA FURAHA; BALI HUDUMU KWA MUDA, IKITUKIA DHIKI AU UDHIA KWA AJILI YA LILE NENO, HUCHUKIZWA. MWINGINE ALISIKIAYE NENO; NA SHUGHULI ZA DUNIA, NA UDANGANYIFU WA MALI HULISONGA LILE NENO, LIKAWA HALIZAI. NA MWINGINE ALISIKIAYE NENO, NA KUELEWA NALO; YEYE NDIYE AZAAYE MATUNDA.
KUSIKIA WATASIKIA, HAWATAELEWA; KUTAZAMA WATATAZAMA, HAWATAONA. MAANA MIOYO YAO IMEKUWA MIZITO HATA WASIJE WAKAONA KWA MACHO YAO, WAKASIKIA KWA MASIKIO YAO, WAKAELEWA KWA MIOYO YAO, WAKAONGOKA, WAKAPONYWA.
MATHAYO 13:3-16
Comments
Post a Comment