UKIAMUA KUOKOKA, OKOKA KWELI.
Neema na iwe kwenu, na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu katika Kristo Yesu.
Nayajua matendo yako, ya kuwa hu baridi wala hu moto; ingekuwa heri kama ungekuwa baridi au moto; Basi, kwa sababu una uvuguvugu, wala hu baridi wala moto, nitakutapika utoke katika kinywa changu. Mwenye kudhulumu na azidi kudhulumu; na mwenye uchafu na azidi kuwa mchafu; na mwenye haki na azidi kufanya haki; na mtakatifu na azidi kutakaswa. Tazama, naja upesi, na ujira wangu u pamoja nami, kumlipa kila mtu kama kazi yake ilivyo.
Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu; bali yeye hujilinda, wala yule mwovu hamgusi.
Pendo na lisiwe na unafiki tukichukia lililo ovu, tukiambatana na lililo jema. Kwa pendo la udugu, tupendane sisi kwa sisi; kwa heshima tukiwatanguliza wenzetu; kwa bidii, si walegevu; tukiwa na juhudi katika roho zetu; tukimtumikia Bwana; kwa tumaini, tukifurahi; katika dhiki, tukisubiri; katika kusali, tukidumu; kwa mahitaji ya watakatifu, tukifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni tukijitahidi. Tuwabariki wanaotuudhi; tubariki, wala tusilaani.
Kristo Yesu ametupa neno la Mungu; na ulimwengu umetuchukia; kwa kuwa sisi si wa ulimwengu, kama yeye asivyo wa ulimwengu. Na hakuomba kwamba tutolewe katika ulimwengu; bali alimuomba Baba yetu wa mbinguni atulinde na yula mwovu.
Ufunuo wa Yohana 3:15-16,
Ufunuo wa Yohana 22:11-12,
1 Yohana 3:9, 1 Yohana 5:18,
Warumi 12:9-14, Yohana 17:14-15.
Comments
Post a Comment