JE! KRISTO ALISEMA NI LINI ATAKUJA
KUWACHUKUA WAFUASI WAKE?
Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na
kwa Bwana Yesu Kristo.
Tusifadhaike
mioyoni mwetu; tumwamini Mungu, tumwamini na Kristo Yesu. Tupendane . Kama vile
alivyotupenda sisi, nasi tupendane vivyo hivyo. Yeye amekwenda nyumbani kwa
Baba kwenye makao mengi kutuandalia mahali, na atakuja tena kutukaribisha
kwake; ili alipo yeye, nasi tuwepo. Yeye aendapo tunaijua njia. Alisema, yeye
ndiye njia, na kweli, na uzima; mtu haendi kwa Baba, ila kwa yeye aliye njia.
Amani ametuachia; amani yake ametupa; alivyotupa yeye si kama ulimwengu
utoavyo. Tusifadhaike mioyoni mwetu, wala tusiwe na woga.
Mtu akimtumikia,
na amfuate; naye alipo, ndipo na mtumishi wake atakapokuwapo. Tena mtu
akimtumikia, Baba atamheshimu. Yesu akasema, sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo;
sasa mkuu wa ulimwengu huu atatupwa nje. Akaendelea kusema, yeye (Kristo Yesu)
akiinuliwa juu ya nchi, atawavuta wote kwake. Aliyanena hayo akionyesha ni
mauti gani atakayokufa. Na akamwomba Baba hao aliompa wawe pamoja naye po pote
alipo, wapate kuutuzama utukufu wake aliopewa; kwa maana Baba alimpenda kabla
ya kuwekwa msingi ulimwengu. Yeye ni ufufuo na uzima. Amwaminiye yeye,
ajapokufa, atakuwa anaishi milele.
YOHANA 14:1-4,27,
YOHANA 13:34, YOHANA 12:26,31-33,
YOHANA 17:24, YOHANA 11:25-26.
Comments
Post a Comment