JE, KUNA TOFAUTI GANI KATI YA ADAMU
WA KWANZA NA WA PILI?
Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na
kwa Bwana Yesu Kristo.
Ndivyo
ilivyoandikwa, Mtu wa kwanza, Adamu, akawa nafsi iliyo hai; Adamu wa mwisho ni
roho yenye kuhuisha. Lakini hautangulii ule wa roho, bali ule wa asili; baadaye
huja ule wa roho. Mtu wa kwanza atoka katika nchi, ni wa udongo. Mtu wa pili
atoka mbinguni.
Bwana Mungu
akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa
nafsi hai. Kwa maana sisi, wenyeji wetu uko mbinguni; kutoka huko tena
tunamtazamia Mwokozi, Bwana Yesu Kristo; atakayeubadili mwili wetu wa unyonge,
upate kufanana na mwili wake wa utukufu, kwa uweza ule ambao kwa huo aweza hata
kuvitiisha vitu vyote viwe chini yake.
Roho ndiyo itiayo
uzima, mwili haufai kitu; maneno hayo niliyowaambia ni roho, tena ni uzima.
Mungu kwa njia ya Kristo, ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya;
si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha. Basi
"Bwana" ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye
uhuru.
1 Wakorintho 15:45-47, Mwanzo 2:7, Wafilipi 3:20-21,
Yohana 6:63, 2 Wakorintho 3:6,17.
Comments
Post a Comment