JE, NI LINI NA NAMNA GANI WENYE HAKI
WOTE, WALIO HAI NA WAFU, WATAKUWA NA KRISTO?
Neema na iwe
kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na kwa Bwana Yesu Kristo.
Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni
pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao
waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza; kasha walio hai, waliosalia,
watanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili kumlaki Bwana hewani; na hivyo
tutakuwa pamoja na Bwana milele. Walio hai, watakaosalia hata wakati wa kuja kwake
Bwana, hakika hawatawatangulia waliokwisha kulala mauti. Kwa habari ya nyakati
na majira, hamna haja tuandikiwe, maana sisi wenyewe tunajua yakini ya kuwa
siku ya Bwana yaja kama vile mwivi ajavyo usiku.
Inatubidi tujue habari za waliolala mauti,
tusije kuhuzunika kama na wengine wasio na matumaini. Sababu twaamini ya kwamba
Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu
atawaleta pamoja naye. Na siri ni kwamba, hatutalala sote, lakini sote
tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua, wakati wa parapanda ya
mwisho; wafu watafufuliwa, wasiwe na uharibifu, na walio hai watabadilika.
Yanasemwa haya, ya kuwa nyama na damu haziwezi kuurithi ufalme wa Mungu; wala
uharibifu kurithi kutokuharibika. Kristo Yesu ameenda nyumbani kwa Baba kwenye
makao mengi na anatuandalia mahali, atakuja tena atukaribishe kwake; ili alipo yeye, nasi
tuwepo.
Hivyo basi, tusifadhaike mioyoni mwetu;
tumwamini Mungu, pia tumuamini na Kristo Yesu.
1
WATHESALONIKE 4:16-17,1513,14, 1 WATHESALONIKE 5:1-2, 1 WAKORINTHO
15:51-52,50, YOHANA 14:2-3,1.
Comments
Post a Comment