JE, NI NANI AMETURUDISHIA ULE UZIMA
WA MILELE, WALE TUAMINIO?
Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na
kwa Bwana Yesu Kristo.
Tumefufuliwa
pamoja na Kristo; tuyafikiri yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi. Kwa maana
tulikufa, na uhai wetu umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu. Kristo
atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo nasi tutafunuliwa pamoja naye katika
utukufu. Sisi tulioifia dhambi tutaishije katika dhambi? Je, tudumu katika
dhambi ili neema izidi kuwa nyingi? Hasha; tulizikwa pamoja naye Kristo kwa
njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu
kwa njia ya utukufu wa Baba, hivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.
Mungu, kwa kuwa ni
mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda, hata tulipokuwa wafu kwa
sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo, yaani tumeokolewa kwa
neema. Akatufufua pamoja naye Kristo, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu
wa roho, katika Kristo Yesu; ili zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema
yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. Tumeokolewa kwa
neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zetu, ni kipawa cha
Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
Tu kazi ya Mungu,
na tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu
aliyatengeneza ili tuenende nayo.
WAKOLOSAI 3:1-4, WARUMI 6:1-4, WAEFESO 2:4-10.
Comments
Post a Comment