JE! NI WAKATI GANI WAAMINIO WATAPOKEA
KUTOKUHARIBIKA?
Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na
kwa Bwana Yesu Kristo.
Mungu na
ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. Nyama na damu haziwezi
kuurithi ufalme wa Mungu; wala uharibifu kurithi kutokuharibika; vyakula ni kwa
tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili,tumbo na
vyakula. Tuangalie, tunaambiwa sisi siri; hatutalala sote, lakini sote
tutabadilika, kwa dakika moja, kufumba na kufumbua,wakati wa parapanda ya
mwisho; maana parapanda italia, na wafu watafufuliwa kwanza, wasiwe na uharibifu, na ambao
hawajalala nao watabadilika. Huu uharibikao ni sharti uvae kutokuharibika, na
huu wa kufa uvae kutokufa.
Nyumba ya maskani
yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba
isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni. Sisi tulio katika maskani hii
twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile
kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima.
Twaambiwa haya kwa
neno la Bwana, wao watakaokuwa hai, watakaosalia hata wakati wa kuja kwake
Bwana, hawatawatangulia wao waliokwisha
kulala mauti. Bwana atashuka mwenyewe kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na
sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo
watafufuliwa kwanza. Kisha walio hai, waliosalia, watanyakuliwa pamoja nao
katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani kwa pamoja; na hivyo tutakuwa pamoja
na Bwana milele. Tufarijiane kwa maneno haya.
1 WAKORINTHO 15:57,50-53, 1 WAKORINTHO 6:13,
2 WAKORINTHO 5:1,4, 1 WATHESALONIKE 4:15-17.
Comments
Post a Comment