MWOKOZI ALISEMA ALIPAKWA MAFUTA ILI
AFANYE NINI?
Neema na iwe kwetu na amani, zitokazo kwa Mungu Baba yetu na
kwa Bwana Yesu Kristo.
Aliingia katika
sinagogi kama ilivyokuwa desturi yake; akapewa chuo cha nabii Isaya, akatafuta
mahali palipoandikwa, “Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta
kuwahuburi maskini habari njema. Amenituma kuwatangazia wafungwa kufunguliwa
kwao, na vipofu kupata kuona tena, kuwaacha huru waliosetwa, na kutangaza mwaka
wa Bwana uliokubaliwa.” Watu waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho;
akawaambia, Leo maandiko haya yametimia masikioni mwenu; nao wakastaajabu kwa
maneno ya neema yaliyotoka kinywani mwake.
Mungu alimtia Yesu
mafuta kwa Roho Mtakatifu na nguvu; naye akazunguka huko na huko, akitenda kazi
njema na kuponya wote walioonewa na ibilisi; kwa maana Mungu alikuwa pamoja
naye. Yesu alipokwisha kubatizwa, mara akapanda kutoka majini; na tazama,
mbingu zikamfunukia, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua, akija juu yake;
na sauti kutoka mbinguni ikisema, Huyu ni Mwanangu, mpendwa wangu,
ninayependezwa naye.
LUKA 4:16-22, MATENDO YA MITUME 10:38, MATHAYO 3:16-17.
Comments
Post a Comment