Skip to main content

Posts

Showing posts from August, 2019

AJAYE ANAKUJA, HATAKAWIA.

AJAYE ANAKUJA, HATAKAWIA Basi msiutupe ujasiri wenu, kwa maana una thawabu kuu. Maana mnahitaji saburi, ili kwamba mkiisha kuyafanya mapenzi ya Mungu mpate ile ahadi. Kwa kuwa bado kitambo kidogo sana, Yeye ajaye atakuja, wala hatakawia. Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Waebrania 10:35-38 1. Mnahitaji saburi, msiutupe ujasiri wenu. 2. Ili mpate ile ahadi, mfanye mapenzi ya Mungu. 3. Bado kitambo kidogo atakuja, hatakawia. 4. Mwenye haki aishi kwa imani, hana furaha na anayesita-sita. Mbarikiwe sana.

ZAIDI YA KUSHINDA

ZAIDI YA KUSHINDA Lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu. Warumi 8:37-39

FIKIRA ZAO JUU YAKO

FIKIRA ZAO JUU YAKO Nalifurahi sana katika Bwana, kwa kuwa sasa mwisho mmehuisha tena fikira zenu kwa ajili yangu, kama vile mlivyokuwa mkinifikiri hali yangu lakini hamkupata nafasi. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu. Wafilipi 4:10,12,13

MTU ASIJE AKAJISIFU

MTU ASIJE AKAJISIFU hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Waefeso 2:5,8,9 Amani na Upendo wa Mungu uwe pamoja nanyi watoto wa Mungu.Tulikuwa wafu sababu ya makosa yetu, ila tumehuishwa pamoja na Kristo. Tumeokolewa kwa neema kwa njia ya imani, ambayo ni kipawa cha Mungu wala si kwa nafsi zetu, hivyo tusije tukajisifu. Mbarikiwe sana.

CHUKI NI UUAJI

CHUKI NI UUAJI Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji: nanyi mnajua ya kuwa kila mwuaji hana uzima wa milele ukikaa ndani yake. Sisi tunajua ya kuwa tumepita toka mautini kuingia uzimani, kwa maana twawapenda ndugu. Yeye asiyependa, akaa katika mauti. 1 Yohana 3:15,14

MWITO MTAKATIFU TANGU MILELE

MWITO MTAKATIFU TANGU MILELE. ambaye alituokoa akatuita kwa mwito mtakatifu, si kwa kadiri ya matendo yetu sisi, bali kwa kadiri ya makusudi yake yeye na neema yake. Neema hiyo tulipewa katika Kristo Yesu tangu milele, 2 Timotheo 1:9 1. Alituokoa, akatuita. 2. Mwito mtakatifu. 3. Kadri ya makusudi yake. 4. Kadri ya neema yake. 5. Neema tulipewa katika Kristo Yesu. 6. Tulipewa tangu milele. Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Yeremia 1:5

KUFIKIRI KWAKO KUBADILIKE

KUFIKIRI KWAKO KUBADILIKE Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Warumi 12:1,2 17 Basi nasema neno hili, tena nashuhudia katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waenendavyo, katika ubatili wa nia zao; Bali ninyi, sivyo mlivyojifunza Kristo; ikiwa mlimsikia mkafundishwa katika yeye, kama kweli ilivyo katika Yesu, mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani, unaoharibika kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya; na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli. Waefeso 4:17,20-24

ENENDA NURUNI

ENENDA NURUNI bali tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote. 1 Yohana 1:7 Enyi wa nyumba ya Israeli, njoni, twende katika nuru ya Bwana. Isaya 2:5 Neno lako ni taa ya miguu yangu, Na mwanga wa njia yangu. Kufafanusha maneno yako kwatia nuru, Na kumfahamisha mjinga. Zaburi 119:105-130

KWA NEEMA SI KWA MATENDO

KWA NEEMA, SI KWA MATENDO. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Waefeso 2:4,5,8,9

JIFUNZE KUPOKEA KWA KUTOA

JIFUNZE KUPOKEA KWA KUTOA      ( NYWESHA, UNYWESHWE ) Kuna atawanyaye, lakini huongezewa zaidi; Kuna azuiaye isivyo haki, lakini huelekea uhitaji. Nafsi ya mtu mkarimu itawandishwa; Anyweshaye atanyweshwa mwenyewe. Awanyimaye watu nafaka, watu watamlaani; Auzaye nafaka, baraka itakuwa kichwani pake. Atafutaye mema kwa bidii hutafuta fadhili; Atafutaye madhara, hayo yatamjia. Azitegemeaye mali zake ataanguka; Mwenye haki atasitawi kama jani. Mithali 11:24-28

KIBALI MBELE ZA BWANA

OMBA KIBALI MBELE ZA BWANA Maneno ya kinywa changu, Na mawazo ya moyo wangu, Yapate kibali mbele zako, Ee Bwana, Mwamba wangu, na mwokozi wangu. Umzuie mtumishi wako asitende mambo ya kiburi, Yasinitawale mimi. Ndipo nitakapokuwa kamili, Nami nitakuwa safi, sina kosa lililo kubwa. Zaburi 19:14-13

NABII MKE

TAFAKARI: NABII MKE Palikuwa na nabii mke, jina lake Ana, binti Fanueli, wa kabila ya Asheri, na umri wake ulikuwa miaka mingi, alikuwa amekaa na mume miaka saba baada ya uanawali wake. Naye ni mjane wa miaka themanini na minne; haondoki katika hekalu, ila huabudu usiku na mchana kwa kufunga na kuomba. Luka 2:36-37

AMANI YAKO NA HAKI YAKO

AMANI YAKO NA HAKI YAKO Nikaribieni, sikieni haya; tokea mwanzo sikunena kwa siri; tangu yalipokuwapo, mimi nipo; na sasa Bwana MUNGU amenituma, na roho yake. Bwana, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni Bwana, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari; Isaya 48:16-18 Laiti wangekuwa na moyo kama huu ndani yao sikuzote, wa kunicha, na kushika amri zangu zote sikuzote, wapate kufanikiwa wao na watoto wao milele! Kumbukumbu la Torati 5:29

TAFAKARI: MAJARIBUNI

TAFAKARI: MAJARIBUNI Mjaribu akamjia akamwambia, Ukiwa ndiwe Mwana wa Mungu, amuru kwamba mawe haya yawe mikate. Mathayo 4:3 Kwa hiyo mimi nami nilipokuwa siwezi kuvumilia tena, nalituma mtu ili niijue imani yenu, asije yule mjaribu akawajaribu, na taabu yetu ikawa haina faida. 1 Wathesalonike 3:5 Mtu ajaribiwapo, asiseme, Ninajaribiwa na Mungu; maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu. Yakobo 1:13 Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. 1 Wakorintho 10:13 Kisha Yesu alipandishwa na Roho nyikani, ili ajaribiwe na Ibilisi. Mathayo 4:1 Bwana asifiwe watu wa Mungu. Wapendwa, Mungu hajaribu wala hajaribiwi ila hutuongoza kwenye majaribu ili kutuimarisha kiimani. Anayetujaribu ni yule muovu. Mbarikiwe sana, Amina.

SIO UAMINIFU

TAFAKARI: SIO UAMINIFU Bwana Mungu akawafanyia Adamu na mkewe mavazi ya ngozi, akawavika. Bwana Mungu akasema, Basi, huyu mtu amekuwa kama mmoja wetu, kwa kujua mema na mabaya; na sasa asije akanyosha mkono wake akatwaa matunda ya mti wa uzima, akala, akaishi milele; Basi akamfukuza huyo mtu, akaweka Makerubi, upande wa mashariki wa bustani ya Edeni, na upanga wa moto uliogeuka huko na huko, kuilinda njia ya mti wa uzima. Mwanzo 3:21,22,24 Bwana asifiwe watu wa Mungu. Upendo, uvumilivu na kusamehe, vyote hivyo sio uaminifu. Unaweza kupendwa, kuvumiliwa na kusamehewa lakini usiaminike. Ni kazi yako kufanya uaminike. Uaminifu ni kulikubali  kosa, kujutia na kukiri kutolirudia hilo kosa ulilolifanya, kutolirudia kabisa na kufanya kila namna usifanye makosa mengine tena tofauti na hilo. Tunaona Mungu hapa bado aliwapenda watu wake pamoja na kosa lao, akawafanyia mavazi ya ngozi akawavika. Ila kwa sababu ya matunda ya mti wa uzima, akuwaamini, akawafukuza pale bustanini. Wapendwa ...

MUNGU NI MWAMINIFU

TAFAKARI: MUNGU NI MWAMINIFU Jaribu halikuwapata ninyi, isipokuwa lililo kawaida ya wanadamu; ila Mungu ni mwaminifu; ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo; lakini pamoja na lile jaribu atafanya na mlango wa kutokea, ili mweze kustahimili. 1 Wakorintho 10:13 Lakini Bwana ni mwaminifu, atakayewafanya imara na kuwalinda na yule mwovu. 2 Wathesalonike 3:3

MAPENZI YAKE

TAFAKARI: MAPENZI YAKE Kwa kuwa mimi sikushuka kutoka mbinguni ili niyafanye mapenzi yangu, bali mapenzi yake aliyenipeleka. Yohana 6:38 Neema, Rehema na Upendo wa Mungu zisiwapungukie. Ili uwe mkamilifu ni lazima udumu katika mapenzi yake baba yetu wa mbinguni na siyo mapenzi yako mwenyewe. Ndio maana tunaomba ufalme wake uje ili mapenzi yake yatimizwe hapa duniani kama mbinguni, na sio mapenzi yetu yatimizwe. Mbarikiwe sana.

IMANI NI LAZIMA

TAFAKARI: IMANI NI LAZIMA Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza; kwa maana mtu amwendeaye Mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao. Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana. Waebrania 11:6,1 Bali kila anisikilizaye atakaa salama, Naye atatulia bila kuogopa mabaya. Mithali 1:33

MUNGU ANAKAA NDANI YAKO

TAFAKARI. MUNGU ANAKAA NDANI YETU. Wapenzi, mioyo yetu isipotuhukumu, tuna ujasiri kwa Mungu; na lo lote tuombalo, twalipokea kwake, kwa kuwa twazishika amri zake, na kuyatenda yapendezayo machoni pake. Na hii ndiyo amri yake, kwamba tuliamini jina la Mwana wake Yesu Kristo, na kupendana sisi kwa sisi, kama alivyotupa amri. Naye azishikaye amri zake hukaa ndani yake yeye naye ndani yake. Na katika hili tunajua ya kuwa anakaa ndani yetu, kwa huyo Roho aliyetupa. 1 Yohana 3:21-24

INGEWALAZIMU KUTOKA DUNIANI

TAFAKARI: INGEWALAZIMU KUTOKA DUNIANI Sisemi msichangamane kabisa na wazinzi wa dunia hii, au na wenye kutamani, au na wanyang'anyi, au na wenye kuabudu sanamu; maana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia. 1 Wakorintho 5:10 Maneno hayo aliyasema Yesu; akainua macho yake kuelekea mbinguni, akasema, Baba, saa imekwisha kufika. Mtukuze Mwanao, ili Mwana wako naye akutukuze wewe; Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Yohana 17:1,15-16

NAFSI KATIKA NENO

TAFAKARI: NAFSI KATIKA NENO Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 2 Timotheo 3:16 Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo. Waebrania 4:12 Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai. Mwanzo 2:7 Na macho yake yalikuwa kama mwali wa moto, na juu ya kichwa chake vilemba vingi; naye ana jina lililoandikwa, asilolijua mtu ila yeye mwenyewe. Naye amevikwa vazi lililochovywa katika damu, na jina lake aitwa, Neno la Mungu. Ufunuo wa Yohana 19:12-13 Yesu akajibu, akamwambia, Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake. Yohana 14:23 Bwana asifiwe watu wa Mungu. Tafaka...

KUTAFAKARI

TAFAKARI: KUTAFAKARI Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mchana na usiku, upate kuangalia kutenda sawasawa na maneno yote yaliyoandikwa humo; maana ndipo utakapoifanikisha njia yako, kisha ndipo utakapositawi sana. Yoshua 1:8 Namshuhudia kila mtu ayasikiaye maneno ya unabii wa kitabu hiki, Mtu ye yote akiyaongeza, Mungu atamwongezea hayo mapigo yaliyoandikwa katika kitabu hiki. Ufunuo wa Yohana 22:18 Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Warumi 10:17 Bwana asifiwe watu wa Mungu. Ili kusitawi sana, inabidi kutafakari Neno la Mungu mchana na usiku, bila kubadili chochote kwa kuongeza au kupunguza. Na ili ukue kiimani ni kulisikia neno la Mungu. Hivyo unaposoma Neno la Mungu mahali popote au unaposikia kwa mtu yoyote, SIKILIZA NA TAFAKARI nini Mungu anasema na wewe kupitia hilo neno. Mbarikiwe sana na muwe na siku njema.

MAFUNDISHO YA WANADAMU

TAFAKARI: MAFUNDISHO YA WANADAMU Basi ikiwa mlikufa pamoja na Kristo mkayaacha yale mafundisho ya awali ya ulimwengu, kwa nini kujitia chini ya amri, kama wenye kuishi duniani, Msishike, msionje, msiguse; (mambo hayo yote huharibika wakati wa kutumiwa); hali mkifuata maagizo na mafundisho ya wanadamu? Mambo hayo yanaonekana kana kwamba yana hekima, katika namna ya ibada mliyojitungia wenyewe, na katika kunyenyekea, na katika kuutawala mwili kwa ukali; lakini hayafai kitu kwa kuzizuia tamaa za mwili. Wakolosai 2:20-23 Basi kama mlivyompokea Kristo Yesu, Bwana, enendeni vivyo hivyo katika yeye; Maana katika yeye unakaa utimilifu wote wa Mungu, kwa jinsi ya kimwili. Na ninyi mmetimilika katika yeye aliye kichwa cha enzi yote na mamlaka. Wakolosai 2:6,9,10

TUMJUE YEYE

TAFAKARI: TUMJUE YEYE Na uzima wa milele ndio huu, Wakujue wewe, Mungu wa pekee wa kweli, na Yesu Kristo uliyemtuma. Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Uwatakase kwa ile kweli; neno lako ndiyo kweli. Yohana 17:3,14,17 Nasi twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, naye ametupa akili kwamba tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, yaani, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye Mungu wa kweli, na uzima wa milele. 1 Yohana 5:20

WATOTO WA MUNGU

TAFAKARI: WATOTO WA MUNGU Bali wote waliompokea aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio jina lake; waliozaliwa, si kwa damu, wala si kwa mapenzi ya mwili, wala si kwa mapenzi ya mtu, bali kwa Mungu. Yohana 1:12-13 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba. Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu; na kama tu watoto, basi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Warumi 8:14-17

MSHITAKI WENU

TAFAKARI: MSHITAKI WENU Ilikuwa, siku moja ambayo hao wana wa Mungu walikwenda kujihudhurisha mbele za Bwana, Shetani naye akaenda kati yao. Bwana akamwuliza Shetani, Umetoka wapi wewe? Ndipo Shetani akamjibu Bwana, na kusema, Natoka katika kuzunguka-zunguka duniani, na katika kutembea huku na huku humo. Lakini nyosha mkono wako sasa, uyaguse hayo yote aliyo nayo, naye atakukufuru mbele za uso wako. Bwana akamwambia Shetani, Tazama, yote aliyo nayo yamo katika uwezo wako; lakini usinyoshe mkono wako juu yake yeye mwenyewe. Basi Shetani akatoka mbele za uso wa Bwana. Ayubu 1:6,7,11,12 Mwe na kiasi na kukesha; kwa kuwa mshitaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka-zunguka, akitafuta mtu ammeze. 1 Petro 5:8

MJUAO HAKI

TAFAKARI: MJUAO HAKI Nisikilizeni, ninyi mjuao haki, watu ambao mioyoni mwenu mna sheria yangu; msiogope matukano ya watu, wala msifadhaike kwa sababu ya dhihaka zao. Maana nondo itawala kama vazi, na funza atawala kama sufu; bali haki yangu itakuwa ya milele, na wokovu wangu hata vizazi vyote. Inueni macho yenu mbinguni, mkaitazame nchi chini; maana mbingu zitatoweka kama moshi, na nchi itachakaa kama vazi, nao wakaao ndani yake watakufa kadhalika; bali wokovu wangu utakuwa wa milele, na haki yangu haitatanguka. Isaya 51:7-8,6

TAFAKARI: WAKIWATUKANA

TAFAKARI: WAKIWATUKANA Basi kwa kuwa Kristo aliteswa katika mwili wake, ninyi nanyi jivikeni silaha ya nia ile ile; kwa maana yeye aliyeteswa katika mwili ameachana na dhambi. Tangu sasa msiendelee kuishi katika tamaa za wanadamu, bali katika mapenzi ya Mungu, wakati wenu uliobaki wa kukaa hapa duniani. Maana wakati wa maisha yetu uliopita watosha kwa kutenda mapenzi ya Mataifa; kuenenda katika ufisadi, na tamaa, na ulevi, na karamu za ulafi, na vileo, na ibada ya sanamu isiyo halali; mambo ambayo wao huona kuwa ni ajabu ya ninyi kutokwenda mbio pamoja nao katika ufisadi ule ule usio na kiasi, wakiwatukana. 1 Petro 4:1-4 Bwana asifiwe watu wa Mungu. Tujivike silaha ya nia ile ile, tukiishi katika mapenzi ya Mungu muda uliobaki hapa duniani. Maisha ya kutenda mapenzi ya Mataifa, kuenenda katika njia potofu, imetosha. Watawatukana, ila msiogope. Nao watatoa hesabu kwake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. Lakini mwisho wa mambo yote umekaribia; basi, iweni na aki...

TAFAKARI: JIAMINI NA JITAMBUE

Kama Mkristo uliyeokoka, ni lazima ujitambue wewe ni nani kwa sasa. Ni nini kilifanyika baada ya kumkubali Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Baada ya kuamini alifufuka kutoka wafu. Haiwezekani una AK47, ukakimbizwa na mtu mwenye rungu. Tatizo kubwa watu wanamiliki silaha nzito lakini hawajijui. Mkristo unalogwa? Kwa nini? Mfano mkutano wa injili unazuiwa na wachawi, sio kweli. Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; Waefeso 2:4-6   Nini kimefanyika sasa baada ya hayo, na kwa nini tuna nguvu ya ajabu katika ulimwengu wa Roho. aliotenda katika Kristo alipomfufua katika wafu, akamweka mkono wake wa kuume katika ulimwengu wa roho; juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na kila jina litajwalo, ...

TAFAKARI: CHUMVI NA NURU

TAFAKARI: CHUMVI NA NURU Heri ninyi watakapowashutumu na kuwaudhi na kuwanenea kila neno baya kwa uongo, kwa ajili yangu. Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikiwa imeharibika itatiwa nini hata ikolee? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu. Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji hauwezi kusitirika ukiwa juu ya mlima. Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni. Mathayo 5:11,13,14,16 Bwana asifiwe watu wa Mungu. Chumvi na Nuru; kwa matendo yetu mema Baba yetu wa mbinguni atukuzwe. Mtashutumiwa, mtaudhiwa na mtanenewa mabaya kwa uongo, lakini mzidi katika kutenda mema. Mbarikiwe sana na muwe na siku njema.

TAFAKARI: ALIKUJUA, ALIKUTAKASA

TAFAKARI: ALIKUJUA, ALIKUTAKASA Neno la Bwana lilinijia, kusema, Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa. Lakini Bwana akaniambia, Usiseme, Mimi ni mtoto; maana utakwenda kwa kila mtu nitakayekutuma kwake, nawe utasema kila neno nitakalokuamuru. Usiogope kwa sababu ya hao maana mimi nipo pamoja nawe nikuokoe, asema Bwana. Yeremia 1:,4,5,7,8

TAFAKARI: MPINGENI SHETANI

TAFAKARI: MPINGENI SHETANI Au mwadhani ya kwamba maandiko yasema bure? Huyo Roho akaaye ndani yetu hututamani kiasi cha kuona wivu? Lakini hutujalia sisi neema iliyozidi; kwa hiyo husema, Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu. Basi mtiini Mungu. Mpingeni Shetani, naye atawakimbia. Mkaribieni Mungu, naye atawakaribia ninyi. Itakaseni mikono yenu, enyi wenye dhambi, na kuisafisha mioyo yenu, enyi wenye nia mbili. Yakobo 4:5-8