NI NANI PEKEE ANAWEZA KUWA MSHINDI? Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu? 1 Yohana 5:5 Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. 1 Yohana 3:9 Bali hadithi za kizee, zisizokuwa za dini, uzikatae; nawe ujizoeze kupata utauwa. Kwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye. 1 Timotheo 4:7-8 Hivyo, kupata ushindi, amini kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu na ndiye Kristo, na usitende dhambi. Kama umezaliwa na Mungu, jizoeze kupata utauwa sababu ya uzima wa sasa na wa baadae. Amani, Upendo, Neema na Rehema za Mungu zidumu pamoja nanyi.
KARIBU KWENYE BLOG YENYE TAFAKARI NA MASOMO YA NENO LA MUNGU. MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI; NDIVYO MEMA YATAKAVYOJIA. NENO LAKE ULIWEKE MOYONI MWAKO.