JE, TUNAPASWA KUTUBU KWA NANI, NA KUONYESHA IMANI KWA NANI? nikiwashuhudia Wayahudi na Wayunani wamtubie Mungu, na kumwamini Bwana wetu Yesu Kristo. Matendo ya Mitume 20:21 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Baada ya Yesu kutoka nyikani alikoongozwa na Roho, akiwako huko siku arobaini, hali akijaribiwa na shetani, alikokuwa pamoja na wanyama wa mwitu na malaika wakiwa wanamhudumia; alienda Galilaya akihubiri Habari Njema ya ufalme wa Mungu akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili. Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia. Mathayo 4:17 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana; Matendo ya Mitume 3:19 hali tukijua ya kuwa mwanadamu hahesabiwi haki kwa matendo ya sheria, bali kwa imani ya Kristo Yesu; sisi tulimwamini Kristo Yesu ili tuhesabiwe haki kwa imani ya Kris...
KARIBU KWENYE BLOG YENYE TAFAKARI NA MASOMO YA NENO LA MUNGU. MJUE SANA MUNGU ILI UWE NA AMANI; NDIVYO MEMA YATAKAVYOJIA. NENO LAKE ULIWEKE MOYONI MWAKO.