Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2020

JE, WATU WAKISHAKUWA WANAFUNZI WA KRISTO, WANATAKIWA KUWA NA NIA GANI?

JE, WATU WAKISHAKUWA WANAFUNZI WA KRISTO, WANATAKIWA KUWA NA NIA GANI? Iweni na nia iyo hiyo ndani yenu ambayo ilikuwamo pia ndani ya Kristo Yesu; Wafilipi 2:5 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Ikiwako faraja ya Kristo, ushirika wa Roho wa Mungu, hutuma na rehema, ijalizeni furaha ya Kristo ili mwe na nia moja, mapenzi mamoja, roho moja, mkinia mamoja; wala msitende neno lolote kwa majivuno ila kwa unyenyekevu, na kila mtu asiangalie mambo yake mwenyewe bali pia na aangalie mambo ya wengine. Kristo, mwanzo alikuwa yuna namna ya Mungu, na akaona kuwa sawa na Mungu ni kitu cha kushikamana nacho; akajifanya hana utukufu, akatwaa namna ya utumwa , akawa mfano wa mwanadamu, akijinyenyekeza na kuwa na utii hata mauti ya msalaba. Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; Warumi 12:10 Mtu asitafute faida yake mwenyewe, bali ya mwenzake. vile vile kama mimi niwapendezavyo watu wote katika mambo...

IKIWA MTU HAUFUATI MWILI, NI NAMNA GANI ANAKUWA SALAMA?

IKIWA MTU HAUFUATI MWILI, NI NAMNA GANI ANAKUWA SALAMA? Lakini ikiwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu, ninyi hamwufuati mwili; bali mwaifuata roho. Lakini mtu awaye yote asipokuwa na Roho wa Kristo, huyo si wake. Warumi 8:9 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Mtu anakuwa salama sababu Roho wa Mungu anakaa ndani yake. Nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, na wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Wanaoongozwa na Roho wa Mungu hao ndio wana wa Mungu, na Roho mwenyewe hushuhudia pamoja na roho zetu, ya kuwa sisi tu watoto wa Mungu, warithi w Mungu, turithio pamoja na Kristo, tukiteswa pamoja naye ili tupate na kutukuzwa pamoja naye. Hamjui ya kuwa ninyi mmekuwa hekalu la Mungu, na ya kuwa Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 1 Wakorintho 3:16 Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hakuna mtu anenaye katika Roho wa Mungu, kusema, Yesu amelaaniwa; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu. 1 Wakorintho 12:3

JE, KRISTO HUUNGANISHWA NA WANAFUNZI WAKE KWA MFANO GANI?

JE, KRISTO HUUNGANISHWA NA WANAFUNZI WAKE KWA MFANO GANI? Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Yohana 15:5 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Huunganishwa na wanafuzi wake kwa mfano wa mzabibu na matawi. Yeye ndani yetu na sisi ndani yake. Yeye ndiye ndiye mzabibu, sisi matawi na Baba yetu aliye Mbinguni ndiye mkulima. Kila tawi ndani yake lizaalo hulisafisha lizidi kuzaa, na tawi lisilozaa huliondoa. Wafuasi wake wamekwisha kuwa safi kwa sababu ya neno lake. Tawi haliwezi kuzaa peke yake lisipokaa ndani ya mzabibu, hivyo sisi tusipokaa ndani yake na yeye ndani yetu. Tukikaa ndani yake, na maneno yake yakikaa ndani yetu, lote tutakalo tukiomba tutatendewa. Hivyo hutukuzwa Baba yangu, kwa vile mzaavyo sana; nanyi mtakuwa wanafunzi wangu. Yohana 15:8 Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. 1 Wakor...

JE, KWA NINI ULIMWENGU UNAMCHUKIA MKRISTO WA KWELI?

JE, KWA NINI ULIMWENGU UNAMCHUKIA MKRISTO WA KWELI? Kama mngekuwa wa ulimwengu, ulimwengu ungewapenda walio wake; lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu, bali mimi naliwachagua katika ulimwengu, kwa sababu hiyo ulimwengu huwachukia. Yohana 15:19 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Twajua ulimwengu umemchukia Kristo kabla hata haujawachukia Wakristo wa kweli. Haya yote watatenda kwa ajili ya jina la Kristo kwa kuwa hawamjui Baba aliyempeleka. Yeye amchukiaye Kristo humchukia na Baba yake. Wa dunia hunena ya dunia na dunia huwasikia. Ulimwengu hauwezi kuwachukia Wakristo bila sababu; bali ni sababu ya Kristo kuushuhudia kazi zake ni mbovu. Ndugu zangu, msistaajabu, ulimwengu ukiwachukia. Mimi nimewapa neno lako; na ulimwengu umewachukia; kwa kuwa wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Yohana 17:14 Heri ninyi watu watakapowachukia, na kuwatenga, na kuwashutumu, na kulitupa nje jina lenu kama neno ovu, kwa ajili ya Mwa...

JE, MTU AKIMFUATA KRISTO ANAPATA NINI?

JE, MTU AKIMFUATA KRISTO ANAPATA NINI? Njoni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha. Mathayo 11:28 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Mtu akimfuata Kristo atapata raha nafsini mwake sababu atampumzisha iwapo ana masumbuko na amelemewa na mizigo. Ujitie nira yake na kujifunza kutoka kwake sababu yeye ni mpole na mnyenyekevu wa moyo. Na kuanzia hapo mtu anakuwa mwanafunzi wa Kristo, maana yeye amekabidhiwa vyote na Baba, Bwana wa mbingu na nchi, mambo aliyowaficha wenye hekima na akili. Hakuna amjuaye Mwana, ila Baba; wala hakuna amjuaye Baba, ila Mwana, na ye yote ambaye Mwana apenda kumfunulia. Nira ya Kristo ni laini, na mzigo wake ni mwepesi. Bwana asema hivi, Simameni katika njia kuu, mkaone, mkaulize habari za mapito ya zamani, I wapi njia iliyo njema? Mkaende katika njia hiyo, nanyi mtajipatia raha katika nafsi zenu. Lakini walisema, Hatutaki kwenda katika njia hiyo. Yeremia 6:16 Kw...

AINA MBILI ZA TAFAKARI.

AINA MBILI ZA TAFAKARI. 1. MAWAZO MEMA. (NENO LA MUNGU). Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, Nisije nikakutenda dhambi. Zaburi 119:11 2. MAWAZO MABAYA. (YA YULE MWOVU). Moyo uwazao mawazo mabaya; Miguu iliyo myepesi kukimbilia maovu; Mithali 6:18 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Ukitafakari vema na mawazo mema utatenda mema, bali ukitafakari vibaya na mawazo mabaya utatenda maovu. Tafakari na mawazo yako ndio matendo yako yatakavyokuwa, na matendo yako yanapelekea kuwa tabia yako. Kutafakari neno la Mungu inakupelekea kutenda mema na kunakuepusha kutenda dhambi, lakini unavyotafakari na kuwa na mawazo mabaya inakupelekea kutenda dhambi. Tuangushe mawazo na kila kijiinucho juu ya elimu ya Mungu kwa neno la Mungu maana silaha za vita vyetu si za mwili na zina uwezo katika Mungu wa kuangusha ngome na kuteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo. Kitabu hiki cha torati kisiondoke kinywani mwako, bali yatafakari maneno yake mch...

JE, NI KWA KITENDO GANI NA NINI MTU ANAPATA KWA BWANA YESU?

JE, NI KWA KITENDO GANI NA NINI MTU ANAPATA KWA BWANA YESU? Maana ninyi nyote mliobatizwa katika Kristo mmemvaa Kristo. Wagalatia 3:27 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu. Hapana Myahudi wala Myunani. Hapana mtumwa wala huru. Hapana mtu mume wala mtu mke, ninyi nyote mmekuwa mmoja katika Kristo Yesu. Sisi sote tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake na tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake ili kwa kufufuka kwake sisi tuenende katika upya wa milele. Bali mvaeni Bwana Yesu Kristo, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake. Warumi 13:14

JE, MUNGU AMEWAWEKEA NINI WATAUWA?

JE, MUNGU AMEWAWEKEA NINI WATAUWA? Bali jueni ya kuwa Bwana amejiteulia mtauwa; Bwana atasikia nimwitapo. Zaburi 4:3 Kwa kuwa umelishika neno la subira yangu, mimi nami nitakulinda, utoke katika saa ya kuharibiwa iliyo tayari kuujilia ulimwengu wote, kuwajaribu wakaao juu ya nchi. Ufunuo wa Yohana 3:10 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Atawasikia wawitapo na kuwaokoa na majaribu. Bwana ajua kuwaokoa wataua na majaribu na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hata siku ya hukumu. Mungu ni mwaminifu na hatawaacha mjaribiwe kupita muwezavyo. Na katika jaribu atafanya mlango wa kutokea, ili muweze kustahimili. Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke. 1 Wakorintho 10:12

JE, WATU WA MUNGU WANAITWAJE SASA, NA WALIKUWAJE KABLA YA KUTEULIWA?

JE, WATU WA MUNGU WANAITWAJE SASA, NA  WALIKUWAJE KABLA YA KUTEULIWA? Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu; ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema. 1 Petro 2:9-10 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Wafumbuliwe macho yao, wageuke waiache giza na kuielekea nuru, waziache na nguvu za shetani nakumwelekea Mungu, ili wapate msamaha wa dhambi zao, na urithi miongoni mwao waliotakaswa kwa imani iliyo kwa Kristo Yesu. Mungu alisema, Nuru itang'aa toka gizani mioyoni mwetu, atupe nuru ya elimu ya utukufu wa Mungu katika uso wa Yesu Kristo. Kwa maana zamani tulikuwa giza, sasa tumekuwa nuru katika Bwana, hivyo tuenende kama watoto wa nuru, tupate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya...

JE, NI USHINDI GANI AMBAO HATIMAYE WATAPEWA WALE AMBAO WAMEZALIWA MARA YA PILI?

JE, NI USHINDI GANI AMBAO HATIMAYE WATAPEWA WALE AMBAO WAMEZALIWA MARA YA PILI? Kwa maana kila kitu kilichozaliwa na Mungu huushinda ulimwengu; na huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu. 1 Yohana 5:4 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Aliyezaliwa na Mungu atapewa kuushinda ulimwengu kwa imani. Mwenye kuushinda ulimwengu ni yeye aaminiye ya kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu. Na ushindi unapatikana kwa sababu aliye ndani yetu ni mkuu kuliko aliye katika dunia. Tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na tuwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo. Hayo nimewaambieni mpate kuwa na amani ndani yangu. Ulimwenguni mnayo dhiki; lakini jipeni moyo; mimi nimeushinda ulimwengu. Yohana 16:33

IKIWA KWELI AMEZALIWA NA MUNGU, MTU ATADHIHIRISHA VIPI?

IKIWA KWELI AMEZALIWA NA MUNGU, MTU ATADHIHIRISHA VIPI? Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. 1 Yohana 4:7 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Atadhihirisha kwa upendo alio nao kwa watu wote. Asiyependa hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo. Pendo la Mungu lilionekana kwetu kwa kumtuma Mwanawe pekee ulimwenguni ili tupate uzima wa milele. Si kwamba sisi tulimpenda Mungu, ila yeye alitupenda sisi. Ikiwa Mungu alitupenda sisi kwa kiasi hichi, inatupasa na sisi kupendana. Tukipendana Mungu hukaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu kwa kuwa ametushirikisha Roho wake. Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani ya Mungu, na Mungu hukaa ndani yake. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake. 1 Yohana 4:16,21 Kwa maana jinsi h...

JE, AGANO LA KALE LILIZUNGUMZIA HABARI NJEMA YA UFALME WA MUNGU ?

JE, AGANO LA KALE LILIZUNGUMZIA HABARI NJEMA YA UFALME WA MUNGU ? Na katika siku za wafalme hao Mungu wa mbinguni atausimamisha ufalme ambao hautaangamizwa milele, wala watu wengine hawataachiwa enzi yake; bali utavunja falme hizi zote vipande vipande na kuziharibu, nao utasimama milele na milele. Danieli 2:44 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani. Maongeo ya enzi yake na amani Hayatakuwa na mwisho kamwe, Katika kiti cha enzi cha Daudi na ufalme wake; Kuuthibitisha na kuutegemeza Kwa hukumu na kwa haki, Tangu sasa na hata milele. Naye akapewa mamlaka, na utukufu, na ufalme, ili watu wa kabila zote, na taifa zote, na lugha zote, wamtumikie; mamlaka yake ni mamlaka ya milele, ambayo hayatapita kamwe, na ufalme wake ni ufalme usioweza kuan...

HABARI NJEMA YA UFALME WA MUNGU.

HABARI NJEMA YA UFALME WA MUNGU. Torati na manabii vilikuwapo mpaka Yohana; tangu wakati huo habari njema ya ufalme wa Mungu hutangazwa, na kila mtu hujiingiza kwa nguvu. Luka 16:16 Hata baada ya Yohana kutiwa gerezani, Yesu akaenda Galilaya, akiihubiri Habari Njema ya Mungu, akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili. Marko 1:14-15 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu. Kristo Yesu alipoulizwa na Mafarisayo, Ufalme wa Mungu utakuja lini? Aliwajibu akawaambia, ufalme wa Mungu hauji kwa kuuchunguza; wala hawatasema, Tazama, upo huku, au, kule, kwa maana, tazama, ufalme wa Mungu umo ndani yenu. Akasema tena, mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Si kwa sababu ya matendo ya haki tuliyoyatenda sisi; bali ...

JE, KUZALIWA UPYA HUFANYA MAISHA YA AINA GANI?

JE, KUZALIWA UPYA HUFANYA MAISHA YA AINA GANI? Vivyo hivyo ninyi nanyi jihesabuni kuwa wafu kwa dhambi na walio hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Warumi 6:11 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Mtu anakuwa hai kwa Mungu katika Kristo Yesu. Fahamu kuwa tuliobatizwa katika Kristo Yesu tulibatizwa katika mauti yake. Tulizikwa pamoja naye kwa huo ubatizo, kusudi kama alivyofufuka katika wafu kwa utukufu wa Baba, na sisi tuenende katika upya wa uzima. Tulivyounganika na Kristo katika mfano wa mauti yake, tutaunganika kwa mfano wa kufufuka kwake. tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao. 2 Wakorintho 5:15 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa. 1 Petro 2:24

JE, NI SAHIHI KUMWITA MTU MCHAFU AU NAJISI?

JE, NI SAHIHI KUMWITA MTU MCHAFU AU NAJISI? Sauti ikamjia mara ya pili, ikimwambia, Vilivyotakaswa na Mungu, usiviite wewe najisi. Petro alipokuwa akiingia Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia. Lakini Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwanadamu. Akawaambia, Ninyi mnajua ya kuwa si halali mtu aliye Myahudi ashikamane na mtu aliye wa taifa lingine wala kumwendea, lakini Mungu amenionya, nisimwite mtu awaye yote mchafu wala najisi. Matendo ya Mitume 10:15,25-26,28 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Siyo sahihi, na Mungu alionya, asiitwe mtu awaye yote mchafu wala najisi. Hii ilipelekea Petro kutambua ya kuwa Mungu hana upendeleo na katika kila taifa mtu amchaye Mungu na kutenda haki hukubaliwa na yeye. wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; twawahubiri habari njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mb...

JE, MTU ALIYEZALIWA NA MUNGU ATAIZINGATIA DHAMBI?

JE, MTU ALIYEZALIWA NA MUNGU ATAIZINGATIA DHAMBI? Kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, kwa sababu uzao wake wakaa ndani yake; wala hawezi kutenda dhambi kwa sababu amezaliwa kutokana na Mungu. 1 Yohana 3:9 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Atendaye dhambi afanya uasi, kwa sababu dhambi ni uasi. Na atendaye dhambi ni wa ibilisi, na ibilisi alitenda dhambi tangu mwanzo; hivyo Mwana wa Mungu alidhihirishwa ili azivunje kazi zake huyo ibilisi. Lisilo la haki ni dhambi. Twajua ya kuwa kila mtu aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi; bali yeye aliyezaliwa na Mungu hujilinda, wala yule mwovu hamgusi. 1 Yohana 5:18 Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. 1 Petro 1:23 Mimi siombi kwamba uwatoe katika ulimwengu; bali uwalinde na yule mwovu. Wao si wa ulimwengu, kama mimi nisivyo wa ulimwengu. Yohana 17:15-16

JE, HAKI NI NINI?

JE, HAKI NI NINI? Kwa sababu hiyo, Ee mfalme, shauri langu lipate kibali kwako; ukaache dhambi zako kwa kutenda haki, ukaache maovu yako kwa kuwahurumia maskini; huenda ukapata kuzidishiwa siku zako za kukaa raha. Danieli 4:27 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Kwa hivyo haki inaonekana kabisa ni kinyume cha dhambi; hivyo ni kufanya vema na kutenda mema. Tumieni akili kama ipasavyo, wala msitende dhambi, kwa maana wengine hawamjui Mungu. Kuweni na juhudi nyingi katika kupendana, maana upendano husitiri wingi wa dhambi. kila mmoja kwa kadiri alivyoipokea karama, itumieni kwa kuhudumiana; kama mawakili wema wa neema mbalimbali za Mungu. 1 Petro 4:10 Haja ya mwenye haki ni mema tu; Bali kutaraji kwake mtu mwovu ni ghadhabu. Mithali 11:23

JE, MTU AKIZALIWA MARA YA PILI ATAFANYA NINI?

JE, MTU AKIZALIWA MARA YA PILI ATAFANYA NINI? Kama mkijua ya kuwa yeye ni mwenye haki, jueni ya kuwa kila atendaye haki amezaliwa na yeye. 1 Yohana 2:29 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Kama mtu akizaliwa mara ya pili atakuwa mtenda haki. Atadumu katika kujitakasa kama Baba alivyo mtakatifu. Mtu na asiwadanganye; atendaye haki yu na haki kama yeye alivyo na haki. Mtu ye yote asiyetenda haki hatokani na Mungu, wala asiyempenda ndugu yake, maana tumesikia tangu mwanzo, tupendane sisi kwa sisi. Tazameni, ni pendo la namna gani alilotupa Baba, kwamba tuitwe wana wa Mungu; na ndivyo tulivyo. Kwa sababu hii ulimwengu haututambui, kwa kuwa haukumtambua yeye. 1 Yohana 3:1

JE, MATENDO YA ROHO (TUNDA LA ROHO) NI YAPI?

JE, MATENDO YA ROHO (TUNDA LA ROHO) NI YAPI? Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. Mkiongozwa na Roho, hampo chini ya sheria na walio wa Kristo Yesu wameusulibisha mwili pamoja na mawazo yake mabaya na tamaa zake. Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili. Tutimize maagizo ya torati ndani yetu sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Nia ya roho ni uzima na amani kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli; Waefeso 5:9 Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Wagalatia 5:25 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. 1 Petro 2:11

JE, MATENDO YA MWILI NI YAPI?

JE, MATENDO YA MWILI NI YAPI? Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Basi matendo ya mwili ni dhahiri, ndiyo haya, uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi, husuda, ulevi, ulafi, na mambo yanayofanana na hayo, katika hayo nawaambia mapema, kama nilivyokwisha kuwaambia, ya kwamba watu watendao mambo ya jinsi hiyo hawataurithi ufalme wa Mungu. Wagalatia 5:19-21 "NA MAMBO YANAYOFANANA NA HAYO". Huko nje wako mbwa, na wachawi, na wazinzi, na wauaji, na hao waabuduo sanamu, na kila mtu apendaye uongo na kuufanya. Ufunuo wa Yohana 22:15 Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi. Waefeso 5:6

JE, HIZI MBILI, ROHO NA MWILI ZINAPATANA?

JE, HIZI MBILI, ROHO NA MWILI ZINAPATANA? Kwa sababu mwili hutamani ukishindana na Roho, na Roho kushindana na mwili; kwa maana hizi zimepingana, hata hamwezi kufanya mnayotaka. Wagalatia 5:17 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Tukienenda kwa Roho, hatutazitimiza kamwe tamaa za mwili. Mkiongozwa na Roho, hampoa chini ya sheria. Tukiishi kwa Roho, na tuenende kwa Roho. Mkiishi kwa kufuata mambo ya mwili mwataka kufa; bali mkiyafisha matendo ya mwili kwa Roho, mtaishi. Maana yeye apandaye kwa mwili wake, katika mwili wake atavuna uharibifu; bali yeye apandaye kwa Roho, katika Roho atavuna uzima wa milele. Wagalatia 6:8 Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho. 1 Petro 2:11 Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Warumi 8:14

JE, MTU ANAWEZA KUZALIWA NA ROHO, NA BADO AKAFUATA MAMBO YA MWILI?

JE, MTU ANAWEZA KUZALIWA NA ROHO, NA BADO AKAFUATA MAMBO YA MWILI? Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Yohana 3:6 Kwa maana wale waufuatao mwili huyafikiri mambo ya mwili; bali wale waifuatao roho huyafikiri mambo ya roho. Warumi 8:5 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Hatuna budi kuzaliwa mara ya pili. Aliyezaliwa na roho, hatakiwi kufuata mambo ya mwili. Sheria ya Roho wa uzima ule ulio katika Kristo Yesu inatuweka huru, mbali na sheria ya dhambi na mauti. Ni ili maagizo ya torati yatimizwe ndani yetu sisi tusioenenda kwa kufuata mambo ya mwili, bali mambo ya roho. Nia ya mwili ni mauti; bali nia ya roho ni uzima na amani. Nia ya mwili ni uadui juu ya Mungu, hivyo wale waufuatao mwili hawawezi kumpendeza Mungu. Na Kristo akiwa ndani yenu, mwili wenu umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yenu i hai, kwa sababu ya haki. Kwa kuwa wote wanaoongozwa na Roho wa Mungu, hao ndio wana wa Mungu. Waru...

JE, MTU ANAWEZAJE KUUONA UFALME WA MUNGU?

JE, MTU ANAWEZAJE KUUONA UFALME WA MUNGU? Yesu akajibu, akamwambia, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona ufalme wa Mungu. Yohana 3:3 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Usipoongoka na kuwa kama vitoto, hautaingia kamwe katika ufalme wa mbinguni. Yoyote ajinyenyekeshaye mwenyewe kama mtoto mdogo, huyo ndiye aliye mkuu katika ufalme huo. Na azishike amri. Mtu lazima azaliwe kwa maji na kwa Roho, ili aingie katika ufalme huo. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho. Kwa kuwa mmezaliwa mara ya pili; si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa ile isiyoharibika; kwa neno la Mungu lenye uzima, lidumulo hata milele. 1 Petro 1:23

JE, NI NINI KINAIPA DHAMBI NGUVU YA KUUA?

JE, NI NINI KINAIPA DHAMBI NGUVU YA KUUA? Uchungu wa mauti ni dhambi, na nguvu za dhambi ni torati. 1 Wakorintho 15:56 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Je, torati ni dhambi? Hasha! Tusingalitambua dhambi ila kwa sheria, sababu tusingalijua kutamani, kama torati isingalisema, usitamani. Dhambi bila sheria imekufa, na ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yetu kila namna ya kutamani. Tumekwisha kuwekwa huru mbali na dhambi, tumekuwa watumwa wa haki na kufanywa watumwa wa Mungu. Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema. Warumi 7:12 Basi, dhambi isitawale ndani ya miili yenu ipatikanayo na mauti, hata mkazitii tamaa zake; Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema. Warumi 6:12,14 Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu. Warumi 6:23 Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushind...

JE, MTU AKIWA NDANI YA KRISTO, AMEKUWA NINI?

JE, MTU AKIWA NDANI YA KRISTO, AMEKUWA NINI? Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. 2 Wakorintho 5:17 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. AMEKUWA KIUMBE KIPYA. Hakuna hukumu ya adhabu juu yao walio katika Kristo Yesu, hawafuati mwili bali wafuata roho. Na Kristo akiwa ndani yako, mwili wako umekufa kwa sababu ya dhambi; bali roho yako i hai, kwa sababu ya haki. Kristo Yesu asiyejua dhambi alifanywa kuwa dhambi wa ajili yetu, ili tupate kuwa haki ya Mungu katika yeye. Msiyakumbuke mambo ya kwanza, wala msiyatafakari mambo ya zamani. Na yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi akasema, Tazama, nayafanya yote kuwa mapya. Akaniambia, Andika ya kwamba maneno hayo ni amini na kweli. Ufunuo wa Yohana 21:5 Tangu sasa mtu asinitaabishe; kwa maana ninachukua mwilini mwangu chapa zake Yesu. Wagalatia 6:17

JE, MTU ANAWEZA KUFANYA JUHUDI GANI KUMWENDEA MUNGU BILA MSAADA WA KRISTO?

JE, MTU ANAWEZA KUFANYA JUHUDI GANI KUMWENDEA MUNGU BILA MSAADA WA KRISTO? Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote. Yohana 15:5 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Kristo Yesu ndiye mzabibu wa kweli, na Mungu, Baba yetu ndiye mkulima. Tawi ndani yake lisilozaa huliondoa, na linalozaa hulisafisha lizidi kuzaa. Tumekwisha kuwa safi kwa neno alilotuambia, tukae ndani yake, naye ndani yetu. Tunalo tumaini mbele za Mungu kwa njia ya Kristo, na si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. Maana kama vile mwili ni mmoja, nao una viungo vingi, na viungo vyote vya mwili ule, navyo ni vingi, ni mwili mmoja; vivyo hivyo na Kristo. Basi ninyi mmekuwa mwili wa Kristo, na viungo kila kimoja peke yake. 1 Wakorintho 12:12,27 Hapo hapana Myunani wala Myahudi, kutahiriwa wala ...

JE, NI NANI PEKEE ATARUHUSIWA KUMWONA MUNGU?

JE, NI NANI PEKEE ATARUHUSIWA KUMWONA MUNGU? Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Mathayo 5:8 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu,Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Mtu aliye na mikono safi na moyo mweupe, asiyeiinua nafsi yake kwa ubatili wala hakuapa kwa  hila ndicho kizazi cha wautafutao uso wa Mungu. Hakika Mungu ni mwema kwa hao walio safi mioyo yao. Sasa tu wana wa Mungu, haijadhihirika bado tutakavyokuwa ; lakini tunafahamu kuwa tutafanana naye. Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu Zaburi 51:10 Na kila mwenye matumaini haya katika yeye hujitakasa, kama yeye alivyo mtakatifu. 1 Yohana 3:3

JE, HALI YA ASILI YA BINADAMU NI IPI?

JE, HALI YA ASILI YA BINADAMU NI IPI? kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; Warumi 3:23 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Wote wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo, ambaye Mungu amemuweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake. Ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Kristo Yesu kwa wote waaminio. apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu. Warumi 3:26 Basi tukiisha kuhesabiwa haki itokayo katika imani, na mwe na amani kwa Mungu, kwa njia ya Bwana wetu Yesu Kristo, Warumi 5:1

NEEMA YA MUNGU INATUFUNDISHA NINI?

NEEMA YA MUNGU INATUFUNDISHA NINI? Maana neema ya Mungu iwaokoayo wanadamu wote imefunuliwa; nayo yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia; tupate kuishi kwa kiasi, na haki, na utauwa, katika ulimwengu huu wa sasa; Tito 2:11-12 Ahimidiwe na atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo na Baba yetu aliye mbinguni. Tusiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia; maana mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali tudumu katika kuyafanya mapenzi ya Mungu hata milele. Katika Kristo, kwa damu yake, tunao ukombozi wetu, masamaha ya dhambi, sawasawa na wingi wa neema yake. kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Na usifiwe utukufu wa neema yake, ambayo ametuneemesha katika huyo Mpendwa. Waefeso 1:4,6 Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatoka...